Tutaona na mwarabu leo kama watammudu,ukiona manyoya kaliwa huyo.Sijawahi kuona mashabiki wa ajabu kama mashabiki wa simba. Yaani wanaishangilia timu yoyote inayocheza na yanga kuliko wanavyoishangilia simba kwenye mechi zake.
Simba banaMajungu hayatawasaidia, akichezesha refa wa Tanzania mnadai kahongwa, akichezesha wa nje kapendelea sasa refa atoke wapi??Yaani kipa atoke golini kabla ya penati, eti kwa vile anachezea katimu kadogo ndio aachiwe?? Kweli huu ndio mchango wako wa kukuza soka duni la East Afrika?? Soka la ukanda huu ndio duni kabisa ktk bara la afrika na bado mnataka kulidumaza zaidi? Nyie kama Simba mnafaidika nini kuendeleza majungu na fitina ktk soka? Badilikeni ndugu zangu.Yanga hawakucheza vizuri kabisa jana lakin walishinda ile mechi kihalali kabida. Na isitoshe wale Red Sea ndio walikuwa ovyo kabisa, hata soka lao lilijionyesha wazi kabisa, hawakuwa na uwezo wa kulisogelea goli la Yanga, na walitegemea ngekewa za penati tu, ambazo hata hivyo nazo walitaka kuziharibu. Walionekana waziwazi wanataka kuharibu utaratibu wa kupigiana penati tangu uchaguzi wa goli la kuchezea penati.Nina declare kabisa interest kuwa mimi ni shabiki wa Simba Sports Club ila natoa maoni kama mwananchi mpenda maendeleo ya michezo. Yule Kibendera na pengine mwamuzi wa mechi ya robo fainali iliyowakutanisha Yanga na timu ya Djibuti alifanya upendeleo wa wazi wazi kukataa penalti mbili ambazo kipa wao alizipangua kwa kisingizio cha kuwa kipa anatoka kabla. Kweli nchi zetu za ukanda huu haziwezi kupiga hatua kimichezo kwa vitendo kama hivi. Aibu
Simba fans ndo staili yao hiyo. Wanajua mtu wa kuwatibulia dili zao kisoka ni Yanga tu, na wanajua hawaiamini timu yao uwanjani.Yaani kuna watu hapa ni Simba live live eti wanajiita Yanga damu na kudai kabebwa jana ili aonekane kaongea point. Acha Yanga wabebwe tu, na watabebwa hadi ubingwa.Sijawahi kuona mashabiki wa ajabu kama mashabiki wa simba. Yaani wanaishangilia timu yoyote inayocheza na yanga kuliko wanavyoishangilia simba kwenye mechi zake.
Mkuu ni kweli tugange yajayo lkn jana YANGA walipewa mbeleko kiaina!Hivi mliangalia Replay za ile penati ya Gumbo na Asamoah?.....Mbona ilionekana ni kweli kipa alivuka msitari,alitoka golini kabla refa hajaruhusu penati ipigwe.....Ikumbukwe kwamba penati nazo zina sheria/taratibu zake.......Cha msingi hapa ni kuongelea game ya Simba na El-Mereikh itakuwaje leo......Haya ya Yanga na Red Sea yameshapita,tugange yajayo sasa......
Mtani acha ushabiki, Hata kocha wa Red sea amekiri kuwa kipa wao alikuwa anatoka, tumsifu refa na wasaidizi wake kwa kuwa makini.Nina declare kabisa interest kuwa mimi ni shabiki wa Simba Sports Club ila natoa maoni kama mwananchi mpenda maendeleo ya michezo. Yule Kibendera na pengine mwamuzi wa mechi ya robo fainali iliyowakutanisha Yanga na timu ya Djibuti alifanya upendeleo wa wazi wazi kukataa penalti mbili ambazo kipa wao alizipangua kwa kisingizio cha kuwa kipa anatoka kabla. Kweli nchi zetu za ukanda huu haziwezi kupiga hatua kimichezo kwa vitendo kama hivi. Aibu
Una washanga Simba vipi mashabiki wa Yanga leo utawashangaa pia.....Mimi ni simba lakini napenda tukutane fainali maana najua nyie hamtuwezi...Sijawahi kuona mashabiki wa ajabu kama mashabiki wa simba. Yaani wanaishangilia timu yoyote inayocheza na yanga kuliko wanavyoishangilia simba kwenye mechi zake.
Angalia uwezo mkuu, hakuna mpira nje ya uwanja hivyo tutafutane baada ya mechi ya leo jioni.Manji in action kahonga marefa usishangae akahonga hata dhidi ya st George
Nina declare kabisa interest kuwa mimi ni shabiki wa Simba Sports Club ila natoa maoni kama mwananchi mpenda maendeleo ya michezo. Yule Kibendera na pengine mwamuzi wa mechi ya robo fainali iliyowakutanisha Yanga na timu ya Djibuti alifanya upendeleo wa wazi wazi kukataa penalti mbili ambazo kipa wao alizipangua kwa kisingizio cha kuwa kipa anatoka kabla. Kweli nchi zetu za ukanda huu haziwezi kupiga hatua kimichezo kwa vitendo kama hivi. Aibu
Nami na declare interest ni mshabiki wa Simba na Simba ikifungwa nahuzunika, Kuhusu mechi ya Yanga na Red sea kwa leo sitasema kama refa aliwabeba yanga au la maana hiyo nilisema jana kwenye thread ya mashindano, nitasema hali ilivyokuwa uwanjani na maelezo juu ya utaratibu wa kupiga penati.
Dakika 90 ziliisha sare ya bila kufungana Red sea wakicheza kwa kujilinda kwa ufundi wa hali ya juu kila wanaposhambuliwa na soka la kuvutia pasi za chini chini na kwa kujiamini kwa taratibu sana bila haraka wakiwa katikati ya uwanja au wakati wanashambulia huku Yanga wakitumia mawinga kupiga krosi lakini hadi dakika ya 90 hakuna aliyetoka na ushindi.
Ikafika muda wa penati, kawaida refa anatakiwa aangalie kama kuna timu ina wachezaji pungufu na kama itakuwepo basi refa atamuita nahodha wa timu yenye wachezaji wengi na kumwambia ataje wachezaji ambao hawatapiga penati ili idadi ilingane na timu nyingine na waliozidi watatoka nje, kwa jana hii haikutumika maana wachezaji kwa timu zote walikuwa sawa yaani kumi na moja.
Timu mwenyeji italazimika kuchagua lango lipi litumike, hilo sitalizungumzia.
waamuzi wawili watatumika mwamuzi wa kati na mshika kibendera, kipa hatatakiwa kuvuka mstari wa goli kuingia ndani ya uwanja mpaka wakati mpira unapigwa lakini anaruhusiwa kwenda kushoto, kulia au hata nyuma ya mstari kama atataka, na mpira utakuwa meta 12 kutoka mstari wa goli kuelekea eneo la kuchezea na zitapigwa penati tano za kwanza kwa kila upande.
Hapa kuna mambo kama manne:
1. Mpira unaweza kuingia hapa litakuwa goli,
2. Kipa anaweza kucheza,
3. Mpira unaweza kugonga mwamba (miamba iliyowima au ulio mlalo),
4. Mpira unaweza kutoka kwa maana usilenge goli ukapaaa juu au mpigaji akapiga kushoto au kulia mwa lango.
Ni wakati gani mpigaji atalazimika kurudia, atalazimika kurudia tu pale ambapo golikipa atatoka kabla mpira haujapigwa na akaucheza, lakini kama atatoka na mpira ukaingia litahesabiwa goli na kama atatoka na mpira ukaangukia kwenye option ya 3 au 4 hapo juu basi halitakuwa goli na mpigaji hatarudia.
Kwa issue ya jana, Penati aliyopiga Gumbo ilichezwa na ikarudiwa na penati aliyopiga Asamoah iligonga mwamba na ikarudiwa.
Ukizingatia mambo yote hapo juu basi utaweza kuona kama kulikuwa na upendeleo au la.
Nawasilisha.
Mkuu mimi sijauma uma maneno, wanasema kabla mpira haujapigwa kama atasogea mbele au kusogeza mkuu, hiyo maana yake ni nini pamoja na hayo yote na refa kuwa ameona kwamba golikipa alisogea mbele au alisogeza mguu lakini ataruhusu mpira upigwe lakini itarudiwa tu endapo kipa atacheza na si vinginevyo hapo ndo mwamuzi wa kati alipochemka kwenye penati ya Asamoah lakini ya Gumbo he was right, mshika kibendera kwa pale hana kosa.Masuke, haya ndo mambo ambayo hata serikali yetu tunaipigia kelele mara kwa mara, kutokuwa wawazi. Umesema vizuri waambie wanasimba wenzio kuwa kibendera alifanya kazi yake bara bara kwa kufuata sheria, usiume maneno.
''kabla ya kupuliza filimbi na kabla mpira haujapigwa, kipa akitoa mguu wake, refa ataruhusu mpira upigwe. Kama goli halitafungwa, kiki itarudiwa''
hii ina maana kwamba kama akifunga, ni goli hata kama alitoka mapema. Tena wako precise, hata akitoa mguu tu.
Hizo ndo sheria za FIFA, MSITULETEE SHERIA ZENU ZA MCHANGANI
Mkuu mimi sijauma uma maneno, wanasema kabla mpira haujapigwa kama atasogea mbele au kusogeza mkuu, hiyo maana yake ni nini pamoja na hayo yote na refa kuwa ameona kwamba golikipa alisogea mbele au alisogeza mguu lakini ataruhusu mpira upigwe lakini itarudiwa tu endapo kipa atacheza na si vinginevyo hapo ndo mwamuzi wa kati alipochemka kwenye penati ya Asamoah lakini ya Gumbo he was right, mshika kibendera kwa pale hana kosa.
Duniani kote haki ni kidogo sana, Yanga ni timu kubwa na ina washabiki wengi na mapato ya TFF na CECAFA wanategemea hasa viingilio ukizingatia Castle wenyewe wamejitokeza kudhami mwishoni pengine wametoa hela kidogo kwa sababu bajeti ya kudhamin mashindano ya vilabu ya CECAFA haikuwepo.
Maadam Red sea walishindwa kuwatoa ndani ya dakika 90 basi ilikuwa ni ngumu sana kuwatoa kwenye penati.
Nachelea kusema mambo haya yanaweza kutokea leo kama Simba au El-Mereikh asiposhinda ndani ya dakika 90 lakini ni uhakika na ngome ya Simba na uimara wa Kaseja Mungu saidia Simba ishinde ndani ya dakika 90.