Nami na declare interest ni mshabiki wa Simba na Simba ikifungwa nahuzunika, Kuhusu mechi ya Yanga na Red sea kwa leo sitasema kama refa aliwabeba yanga au la maana hiyo nilisema jana kwenye thread ya mashindano, nitasema hali ilivyokuwa uwanjani na maelezo juu ya utaratibu wa kupiga penati.
Dakika 90 ziliisha sare ya bila kufungana Red sea wakicheza kwa kujilinda kwa ufundi wa hali ya juu kila wanaposhambuliwa na soka la kuvutia pasi za chini chini na kwa kujiamini kwa taratibu sana bila haraka wakiwa katikati ya uwanja au wakati wanashambulia huku Yanga wakitumia mawinga kupiga krosi lakini hadi dakika ya 90 hakuna aliyetoka na ushindi.
Ikafika muda wa penati, kawaida refa anatakiwa aangalie kama kuna timu ina wachezaji pungufu na kama itakuwepo basi refa atamuita nahodha wa timu yenye wachezaji wengi na kumwambia ataje wachezaji ambao hawatapiga penati ili idadi ilingane na timu nyingine na waliozidi watatoka nje, kwa jana hii haikutumika maana wachezaji kwa timu zote walikuwa sawa yaani kumi na moja.
Timu mwenyeji italazimika kuchagua lango lipi litumike, hilo sitalizungumzia.
waamuzi wawili watatumika mwamuzi wa kati na mshika kibendera, kipa hatatakiwa kuvuka mstari wa goli kuingia ndani ya uwanja mpaka wakati mpira unapigwa lakini anaruhusiwa kwenda kushoto, kulia au hata nyuma ya mstari kama atataka, na mpira utakuwa meta 12 kutoka mstari wa goli kuelekea eneo la kuchezea na zitapigwa penati tano za kwanza kwa kila upande.
Hapa kuna mambo kama manne:
1. Mpira unaweza kuingia hapa litakuwa goli,
2. Kipa anaweza kucheza,
3. Mpira unaweza kugonga mwamba (miamba iliyowima au ulio mlalo),
4. Mpira unaweza kutoka kwa maana usilenge goli ukapaaa juu au mpigaji akapiga kushoto au kulia mwa lango.
Ni wakati gani mpigaji atalazimika kurudia, atalazimika kurudia tu pale ambapo golikipa atatoka kabla mpira haujapigwa na akaucheza, lakini kama atatoka na mpira ukaingia litahesabiwa goli na kama atatoka na mpira ukaangukia kwenye option ya 3 au 4 hapo juu basi halitakuwa goli na mpigaji hatarudia.
Kwa issue ya jana, Penati aliyopiga Gumbo ilichezwa na ikarudiwa na penati aliyopiga Asamoah iligonga mwamba na ikarudiwa.
Ukizingatia mambo yote hapo juu basi utaweza kuona kama kulikuwa na upendeleo au la.
Nawasilisha.