CECAFA KAGAME CUP 2011 Finals in Tanzania

CECAFA KAGAME CUP 2011 Finals in Tanzania

Walete hao walete hao El-Mereikh......

Kila la heri watani zangu Simba,leo tupo pamoja mwanzo mwisho....

Dua zangu zote nazielekeza kwa Simba........Funga hao El-Mereikh kombe libaki Tanzania

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu ibariki Simba....

Iwe hivyo kweli............SIMBA MBELE
 
Kelvin Yondan na Amir Maftah wanakatika sana na kuruhusu mashambulizi.....

Mipira mingi inaingilia kwa Amir Maftah............Simba inabidi watulie hasa kwenye kiungo

Dakika ya 15 El-Mereikh 0:1 Simba
 
Nami na declare interest ni mshabiki wa Simba na Simba ikifungwa nahuzunika, Kuhusu mechi ya Yanga na Red sea kwa leo sitasema kama refa aliwabeba yanga au la maana hiyo nilisema jana kwenye thread ya mashindano, nitasema hali ilivyokuwa uwanjani na maelezo juu ya utaratibu wa kupiga penati.Dakika 90 ziliisha sare ya bila kufungana Red sea wakicheza kwa kujilinda kwa ufundi wa hali ya juu kila wanaposhambuliwa na soka la kuvutia pasi za chini chini na kwa kujiamini kwa taratibu sana bila haraka wakiwa katikati ya uwanja au wakati wanashambulia huku Yanga wakitumia mawinga kupiga krosi lakini hadi dakika ya 90 hakuna aliyetoka na ushindi.Ikafika muda wa penati, kawaida refa anatakiwa aangalie kama kuna timu ina wachezaji pungufu na kama itakuwepo basi refa atamuita nahodha wa timu yenye wachezaji wengi na kumwambia ataje wachezaji ambao hawatapiga penati ili idadi ilingane na timu nyingine na waliozidi watatoka nje, kwa jana hii haikutumika maana wachezaji kwa timu zote walikuwa sawa yaani kumi na moja.Timu mwenyeji italazimika kuchagua lango lipi litumike, hilo sitalizungumzia.waamuzi wawili watatumika mwamuzi wa kati na mshika kibendera, kipa hatatakiwa kuvuka mstari wa goli kuingia ndani ya uwanja mpaka wakati mpira unapigwa lakini anaruhusiwa kwenda kushoto, kulia au hata nyuma ya mstari kama atataka, na mpira utakuwa meta 12 kutoka mstari wa goli kuelekea eneo la kuchezea na zitapigwa penati tano za kwanza kwa kila upande.Hapa kuna mambo kama manne:1. Mpira unaweza kuingia hapa litakuwa goli,2. Kipa anaweza kucheza, 3. Mpira unaweza kugonga mwamba (miamba iliyowima au ulio mlalo), 4. Mpira unaweza kutoka kwa maana usilenge goli ukapaaa juu au mpigaji akapiga kushoto au kulia mwa lango.Ni wakati gani mpigaji atalazimika kurudia, atalazimika kurudia tu pale ambapo golikipa atatoka kabla mpira haujapigwa na akaucheza, lakini kama atatoka na mpira ukaingia litahesabiwa goli na kama atatoka na mpira ukaangukia kwenye option ya 3 au 4 hapo juu basi halitakuwa goli na mpigaji hatarudia.Kwa issue ya jana, Penati aliyopiga Gumbo ilichezwa na ikarudiwa na penati aliyopiga Asamoah iligonga mwamba na ikarudiwa.Ukizingatia mambo yote hapo juu basi utaweza kuona kama kulikuwa na upendeleo au la.Yote kwa yote TFF na CECAFA watatengeneza hela nyingi kulingana na kwamba Yanga wanawashabiki wengi pengine kuliko hata washabiki wa Simba.Nawasilisha.
You are very right Mkuu,Penalt kick iliyogonga mwamba haikupaswa kurudiwa. CECAFA na TFF wanaua mpira kwa kuendekeza mapato badala ya kufikiria ubora, aibu sana hii.
 
Iwe hivyo kweli............SIMBA MBELE

Kiungo cha Simba kimepwaya sana dakika 15 za mwanzo......

Dakika ya 18 El-Mereikh 1:0 Simba

El-Mereikh wanakosa goli la wazi hapa........

Pengo la Banka linajionesha dhahiri
 
naona kama vile beki ya simba inashindwa kujipanga vile!!!!

Tatizo linaanzia kwenye kiungo......Pengo la Banka linaonekana,Jery Santo kazidiwa hivyo kuzidisha mashambulizi....

Wakiendelea hivi hali itakuwa mbaya zaidi...
 
Mamir Maftah anaharibu sana leo......

Patrick Mafisango anavuja sana pale kati...
 
Goaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaal

Safi sana

Simba wanapata goli
 
Ni uzembe wa kipa wa El-Mereikh......Kafungwa kizembe sana

Safi sana Ulimboka Mwakingwe.....

Dakika ya 27 El-Mereikh 1:1 Simba
 
Mgosiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Offside.....................
 
Walau sasa...maana nilikuwa natafuta anti-hypertensive

Shukrani kwa kipa Esm El-Hadary......

Simba bado wanafanya uzembe ambao utawagharimu na watajuta.....

Kiungo chao kimepwaya sana......Angalau sasa hivi wanafanya mashambulizi
 
Dakika ya 30 sasa

El-Mereikh 1:1 Simba

Simba taratibu wanabadilika...............
 
Kidogo simba wanaonyesha uhai, Elmelek wamepunguza kasi
 
Dakika ya 35

El-Mereikh 1:1 Simba

Hutu Mgosi naye.................Kanzu za nini?
 
Back
Top Bottom