CECAFA: Rwanda Vs Tanzania Bara

CECAFA: Rwanda Vs Tanzania Bara

Casuist

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2014
Posts
1,189
Reaction score
2,970
Habari wakuu,

Leo ni muendelezo wa kombe la CECAFA na Tanzania bara chini ya Kibadeni inarusha karata nyingine dhidi ya Rwanda. Timu ya taifa ya Rwanda imependeza ndani ya uzi wa njano na Tanzania bara wametinga jezi nyeupe zenye fito za kibluu. Mechi inachezewa mjini Hawassa na sote tuwe pamoja kujuzana yatakayojiri.
=======



00' Kipenga kimepulizwa kuashiria mwanzo wa mchezo
09' Himid Mao amekosa goli baada ya kupiga shuti kali lakini hakuweza kulenga goli
11' Tanzania Bara wanapata kona lakini haikuzaa matunda baada ya kuondolewa na mabeki wa Rwanda
18' Rwanda wamecheza pasi nzuri kuingia boksi la Tanzania lakini wamekwamishwa na mabeki
21' Mugiraneza kadi ya njano baada ya kumuwekea mguu John Boko
22' :A S soccer:Goaaaal, Said Ndemla wa Kilimanjaro stars anapachika goli la kuongoza kupitia mpira wa adhabu
30' Ernest wa Rwanda anakosa goli baada ya kupiga sentimita chache nje ya goli la Tanzania
33' Batista anakosa goli baada ya kuunganisha krosi lakini ilienda nje kidogo
45+2'Mpira unaenda mapumziko

45' Mpira umerejea kumalizia ngw'e ya mwisho ya mchezo, Rwanda imefanya mabadiliko ya wachezaji wawili
49' Kaseke anakosa goli kwa kupiga mpira hafifu baada ya kuwekewa mpira mzuri wa pasi na Maguli
52' Msuva anacheza mpira mzuri na kujaribu kumtupia pasi Maguli, beki ya Rwanda inatibua.
53' Baptist anamuweka chini Himid Mao na kugaagaa chini, Mao anatolewa nje kwa machela.
57' Niyonzima anapewa kadi ya njano baada ya kulalamika kutopewa penati
62' Himid Mao anatolewa tena nje na machelewa
65' Mkude anaingia kuchukua nafasi ya Himid Mao

77' :A S soccer:Msuva anaweka goli la pili kimiani baada ya kipa kutoka golini
88' :A S soccer:Rwanda wanaandika goli kupitia kwa Tuisenge, Rwanda 1-2 Tanzania.
90+2' Kadi ya njano kwa Aishi Manula kwa kupoteza muda
90+4' Mwamuzi anapuliza kipenga kuashiria mwisho wa mchezo, Kiilimanjaro stars wanapata pointi tatu nyingine na kutimiza pointi sita.
 
Last edited by a moderator:
Duh Wazanzibar? Hata hivyo UG,KNY,RWND sio timu ndogo EA kama SOMALIA so hata KLM wana kazi kwa hawa kina NIYONZIMA.
 
Hii team lazima igongwe tu maana hamna namna!
 
Duh!
Hivi kumbe hili kombe limeanza, sikuwa najua hata kidogo! Mbona hakukuwa hata na matangazo ya kutosha kutangaza mashindano? Ile dozi ya Algiers naona bado tunayo!
Haiya, twende kazi, Kilimanjaro nyuka hao Amavubi.
 
Hawa Zanzibar mwakahuu wamekuwaje
Wanawaza Wanajeshi Waliopo Zanzibar Sasa Na Nyambizi Ile Ya Kijeshi Inayoibuka Kila Asubuhi Na Jioni Baharini Unguja Na Pemba. Hofu Yangu Wachezaji Wa Zanzibar Wasije Tu Wakatokomea Huko Huko Addis Ababa.
 
namwona edibili jonas lunyamila akipiga jeramba pale, leo Amavubi kazi wanayo.
 
Back
Top Bottom