Cecafa U20: Tanzania Bara yaitandika Uganda kwa magoli 4 - 2 na kufanikiwa kuingia nusu fainali

Cecafa U20: Tanzania Bara yaitandika Uganda kwa magoli 4 - 2 na kufanikiwa kuingia nusu fainali

Dk 76 Uganda wanasawazisha.....goli linafungwa kizembe kabisa, sijui ni utelezi au uzembe wa kipa....Tanzania 2- 2 Uganda
 
Zanzibar wamefungwa goli 5 na Eritrea katika robo fainali nyingine.
 
Kelvin John Tanzania 3- Uganda 2
 
Dk 90 Gooooooooolaaalllllll
 
Mkuu asante sana
Nimeangalia mechi vizuriiiiiiiiii

Ila kipa alitaka kutuharibia
 
Huyu kipa namuona kama hana utulivu sana golini, inabidi wamuweke sawa.

Kwakweli nilijikuta nimejikunyata ghafla

Kaanua hovyohovyo kitu kikampita wakasawazisha. Iliniuma sana ... kipa aliwapa goli

Bora refa hakuwapa penati isiyokuwa penati tungeharibikiwa
 
Hongera nyingi kwa vijana. Wapambane waje na kikombe kama walivyofanya dada zao kwenye yale mashindano ya cosafa.
 
Ushindi mzuri...tusijidharau Watanzania kwa timu za vijana East Africa hawatugusi sema wakitoka hapa wanapoishia hakujulikani
 
Tanzania huwa tupo vizuri sana kwenye timu za Under Xx

Bahati mbaya hizi timu huwa haziendelezwi kuja kuwa timu ya taifa kubwa...
 
Back
Top Bottom