GE2025 Cecilia Paresso aeleza sababu za kujiunga CCM ambazo ni pamoja na kuvutiwa na sera pamoja na siasa za maridhiano

GE2025 Cecilia Paresso aeleza sababu za kujiunga CCM ambazo ni pamoja na kuvutiwa na sera pamoja na siasa za maridhiano

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mwanasiasa machachari na aliyewahi kuwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Cecilia Paresso, ambaye pia aliweka nia ya kuwania ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivi karibuni, ameeleza sababu za kujiunga na chama hicho ambazo ni pamoja na kuvutiwa na sera pamoja na siasa za maridhiano.

Amesema mengine yaliyomvutia ni kuthamini demokrasia na kuimarisha amani na maendeleo, mambo anayosimamia kwa dhati mgombea kupitia tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amewataka Watanzania kumpigia kura nyingi za ndiyo Dkt. Samia katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu wa 2025 kwa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kupokea kijiti cha uongozi wa nchi yetu wakati ikiwa na miradi mikubwa ya kimkakati ambayo ameiendeleza vizuri kwa manufaa ya Watanzania.

 
Back
Top Bottom