The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 zimezidi kupamba moto huku makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiendelea kufanya mikutano maeneo mbalimbali kusaka kura kwa wagombea.
Cecilia Paresso, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha, ni miongoni mwa makada wa chama wanaozunguka maeneo mbalimbali kunadi sera na kusaka kura za mgombea urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Kombe Jimbo la Kaliua mkoani Tabora leo Ijumaa, Septemba 26, 2025, Paresso amewahimiza wananchi kuichagua CCM akisema ni uamuzi sahihi kwa kuwa wagombea wake wamebeba ajenda ya kulinda, kuthamini utu wa Mtanzania na kuwaletea maendeleo ya haraka.
“Thamani ya Mtanzania na maendeleo yake yapo ndani ya wagombea wa CCM. Nawaomba tuhakikishe tunamchagua kwa kishindo Samia kuwa kiongozi wetu. Huyu mama ana maono, ni mtendaji na anathamini maisha ya watanzania.
“Tuhakikishe tunachagua maendeleo, kwa sababu wote tunaona jinsi sekta ya elimu, afya zilivyopiga hatua kubwa. Wananchi wanataka maendeleo na maendeleo yapo CCM wanafunzi wa shule za msingi na sekondari,” amesema Paresso ambaye alitumia nafasi hiyo kumnadi mgombea ubunge wa Kaliua, Joseph Tama.