Ceferin: Sigombei Fifa ila Infantino ajiuzulu

Ceferin: Sigombei Fifa ila Infantino ajiuzulu

Kadhakan

Senior Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
126
Reaction score
201
Rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA), Aleksander Čeferin, amesema hatagombea urais wa Shirikisho la Soka la Duniani (FIFA) dhidi ya rais wa sasa, Gianni Infantino, lakini amemtaka Kiongozi huyo wa soka kujiuzulu.

Infantino anakabiliwa na shinikizo la kuondoka madarakani kufuatia mpango wake uliositishwa wa kuuza hisa katika Kombe la Dunia kwa wawekezaji binafsi.

Soma pia: Rais wa FIFA Gianni Infantino aitisha kikao cha dharula

Mashirikisho matatu ya soka ya mabara yameulaani mpango huo, yakidai kulikuwa na udanganyifu, huku UEFA ikitishia kususia baadhi ya mashindano ya FIFA.

Akizungumza katika mahojiano na podikasti moja nchini Uingereza, Čeferin amesema Infantino hana tena uungwaji mkono wa wadau wengi wa soka, wakiwemo mashabiki, Wachezaji na Makocha.

Hata hivyo, Čeferin mwenye umri wa miaka 58, amesema hana nia ya kuwania urais wa FIFA kwa sababu anaipenda kazi yake UEFA na pia anataka kuwa na muda wa kufurahia maisha yake.

Infantino amekuwa rais wa FIFA tangu mwaka 2016, huku mwisho wa kuwasilisha fomu za wagombea wa uchaguzi huo ukiwa Novemba 18.


1787573555822.png
 
Hizi kelele za kutaka Infantino ajiuzulu ni kelele za wapiga porojo tu.
 
Back
Top Bottom