Sielewi hilo la Celtel, lakini huu mtindo wa makampuni kubadilisha majina ni ujanja wa kutumia hiyo loophole ya Tax Holiday iliyoanzishwa na serikali ya Mwinyi kuvutia foreign investors. Sidhani kama sheria hii imeshafanyiwa mabadiliko makubwa, labda iwe ni siku za hivi karibuni tu. Jamaa waliojenga Sheraton kwa mara ya kwanza walikuwa wamenunua franchise ya Sheraton International ambayo iliwapa mwanya wa kupata Tax holiday kama investor wa nje. Baada ya muda wa hiyo Tax holiday kukaribia kuisha, ndipo wakanunua franchize ya Royal Palm na kuanza kama foreign investor mpya mwenye kustahili Tax holiday nyingine.
Siamini kuwa Sheraton wa kikweli kweli eti wanaweza kushindwa kuendesha hoteli ile ya Dar es Salaama na kuiuza kwa Royal Palm ambao ni kati competitors wake wakubwa, hapana! hiyo ni vigumu sana katika ulimwengu huu wa mashindano ya kibiashara.
JUZI JUZI tu Richmond wamejifanya kuuza biashara zao kwa Dowans, ingawa sasa tunafahamu kuwa yote hayo ni makampuni ya mtu mmoja. Yote hiyo ni katika harakati za wawezezaji hawa kutumia loophole ziolzoko kwenye sheria zetu.