Cement gani nzuri kwa kufyatulia matofali?

Kuna 32.5....42.5n...42.5r

Hizo siyo aina za cement!
Hizo ni grades za cement, na hiyo N inamaanisha Normal strength, R ikiwa na maana ya rapid strength!
Aina za cement zipo nyingi tu, mfano ni kama hizi:-
Ordinary Portland Cement (OPC),Portland Pozzolana Cement (PPC), Rapid Hardening Cement, Extra Rapid Hardening Cement, Low Heat Cement, Sulfates Resisting Cement, Quick Setting Cement, Blast Furnace Slag Cement...n.k!

Kwa Tz aina kuu ya cement inayozalishwa na kutumika zaidi ni OPC na hata PPC, ambazo huwa zinazalishwa grades
32.5N/ 32.5R,(Cement daraja la chini)
42.5N /42.5R.(cement daraja la juu)
Lakini pia ipo 52.5N/52.5R (ambayoni cement daraja la juu zaidi, kwa tz hii bado haipo).
Cement ambayo ni grade 32.5N/32.5R hii inafaa zaidi kwa matumizi ya plaster na kazi ndogo ndogo ambazo hazihitaji kuhimili uzito mkubwa!
Cement ambayo ni grade 42.5N/42.5 au daraja la juu zaidi inafaa zaidi kwa kazi za zege kama nguzo, bimu, slabu, madaraja n.k kutokana na uimara wake kuwa mkubwa zaidi.

Maana ya herufi N, kama nilivyoeleza ni normal strengh, hii ina maana ili kufikia ubora wake baada ya matumizi huchukua muda kidogo tofauti na cement ambayo ni R-rapid strenght ambayo hii huwahi zaidi kufikia ubora wake baada ya matumizi! Kawaida ubora wake hufikiwa kuanzia siku 2-7.
Hivyo naamini kwa maelezo haya mafupi unaweza kuamua utumie cement yenye grades zipi kwa matumizi gani!
 
Sorry,hv nn tofaut,au maana ya hyo N au R?ni ubora Zaid,au mbwembwe tu...
42.5R - rapid setting cement yaani ikitengenezwa zege inakakamaa fastafasta na kuwa jiwe(initial curing time ni ndogo)
42.5N - hiyo N inasimama badala ya NORMAL, setting time yake ni kawaida ,sio rapid (curring time kubwa) ,zote ni grade maana yake final strength ya zege la 42.5R na 42.5N Inafanana zinatofautiana kwenye curing time tu,42.5 R inakakamaa fastafasta
Hii 42.R Nadhani ndo inatumikaga kujenga coulms sehemu zenye maji
 
Namalizia kufanya finishing nyumba yangu Cement leo hakuna hapa Lindi. Jana nilinunua sehemu ilikuwa 2 nikanunua mfuko 1 elf 16. Nilianza ujenzi Mwaka uliopita mwez wa 12. Cement ilikuwa inauzwa elf 12 sasa hv imepanda

Ni shida sana.
 
It is ✊🏻 again.
 
Heading inajieleza,wala cna la kuongezea,wataalam mkuje kutufafanulia
Inategemea na mahali ulipo kwamaana ya mkoa kama uko sehemu zenye baridi na zenye mchanga wenye tifutifu nyingi kwamaana ya clayer-sand materials tumia pozolana ya Mbeya Cement, ila kama unamchanga mzuri na hali ya hewa ni joto muda mwingi Twigs au Tanga Cement zitakufaa
 
Hizo siyo aina za cement!
Hizo ni grades za cement, na hiyo N inamaanisha Normal strength, R ikiwa na maana ya rapid strength!
Aina za cement zipo nyingi tu, mfano ni kama hizi:-
Ordinary Portland Cement (OPC),Portland Pozzolana Cement (PPC), Rapid Hardening Cement, Extra Rapid Hardening Cement, Low Heat Cement, Sulfates Resisting Cement, Quick Setting Cement, Blast Furnace Slag Cement...n.k!

Kwa Tz aina kuu ya cement inayozalishwa na kutumika zaidi ni OPC na hata PPC, ambazo huwa zinazalishwa grades
32.5N/ 32.5R,(Cement daraja la chini)
42.5N /42.5R.(cement daraja la juu)
Lakini pia ipo 52.5N/52.5R (ambayoni cement daraja la juu zaidi, kwa tz hii bado haipo).
Cement ambayo ni grade 32.5N/32.5R hii inafaa zaidi kwa matumizi ya plaster na kazi ndogo ndogo ambazo hazihitaji kuhimili uzito mkubwa!
Cement ambayo ni grade 42.5N/42.5 au daraja la juu zaidi inafaa zaidi kwa kazi za zege kama nguzo, bimu, slabu, madaraja n.k kutokana na uimara wake kuwa mkubwa zaidi.

Maana ya herufi N, kama nilivyoeleza ni normal strengh, hii ina maana ili kufikia ubora wake baada ya matumizi huchukua muda kidogo tofauti na cement ambayo ni R-rapid strenght ambayo hii huwahi zaidi kufikia ubora wake baada ya matumizi! Kawaida ubora wake hufikiwa kuanzia siku 2-7.
Hivyo naamini kwa maelezo haya mafupi unaweza kuamua utumie cement yenye grades zipi kwa matumizi gani!
Hivi vitu mafundi wanavijua kweli au ndio "uzoefu"?
 
Back
Top Bottom