Cement imepanda bei

evangelical

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2011
Posts
5,035
Reaction score
8,218
Duuh wajenzi tuna shida sana,

Nimekwenda kununua cement Leo.

Hardware 2 wakaniambia hawana cement. Ikabidi niende dukani Kwa mshkaji ninayemfahamu akaanza kulalamika kwamba hauzi sijui anataka afatulie tofali za kuuza.

Nikamkomalia sana na kumdadisi mbona wengine hawana ndipo akanieleza wanazo ila wanazificha wanasikilizia bei mpya kuanzia Leo itajulikana rasmi.

Basi baada ya kumsihi sana kwamba ninakazi naendelea nayo Kwa shingo upande akaniuzia Kwa sh 16500 Kwa mfuko, wakati juzi tu ilikuwa inauzwa sh 14,500 Kwa mfuko.

Na cement inayopatikana sasa ni Dangote 42 only.

Hapa ni DSM sijui huko mikoani itakuwaje.

Kunatatizo gani kwenye viwanda vingine vya cement?
 
Huku kwetu dangote inaenda tsh. 18000/, wiki moja nyuma ilikuwa 16,000.
 
Njoo kwangu Tabata DSM nikuuzie Twiga Cement kwa sh 17,000.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…