Asprin
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 68,223
- 96,083
Kama unataka kutumia kiasi kikubwa na una kampuni ya ujenzi wa nyumba za maghorofa manne kwenda juu, basi ni heri uchue hiyo Cement, changanya na kokoto (Concrete) kwa Ratio watakayosema watengenezaji cement na chukua mawe safi, maji safi na mchanga safi na tengeneza Zege lako na utengeneze Cubes na kisha upeleke UDSM kuzi-Crush.
Matokeo utakayopata yasipishane sana na kiasi walichosema wao. Kumbuka kwamba kwenye SITE, utatumia quality mbaya na hutakuwa na muda wa kutosha kufanya kama ilivyo kwenye SAMPLE.
Ila kwa jengo la ghorofa kuanzia nne kushuka chini, msiwe na wasiwasi, hata hiyo ya 35 sijui mnaweza kuitumia ila cha muhimu mhakikishe mnapima vizuri kokoto mnazoweka na msizidishe maji wala kuweka maji kidogo na kuhakikisha mnashindilia vizuri. Jengo litakuwa poa tu.
Kuna maghorofa nilishaona yamejengwa kwa matofali ya kuchoma na yapo imara tu. Ila kuta zake zinazobeba uzito ni nene sana maana kwa jengo la ghorofa nne, ukuta una kama upana wa mita moja hivi.
Tafadhali kila panapowezekana, tumia Matofali ya kuchoma na epukaneni na Cement maana huwa zinatoa Radiations ambazo si nzuri kwa afya zenu. Na kama walivyosema wengi, CEMENT NUNUA iliyoandikwa MADE IN TANZANIA.
Tuisaidie Nchi yetu kwa kununua vitu MADE IN TANZANIA.
Nakuona fundi mchundo uko kazini.