CEO Simba atema cheche kwa Mkude

CEO Simba atema cheche kwa Mkude

Baada ya kikosi cha Simba kurejea jijini Dar es Salaam jana, kwa sasa kinachosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka nchini, hasa Wanamsimbazi, ni nini kitaendelea kuhusiana na kiungo wao, Jonas Mkude ambaye alidaiwa kukacha safari ya Kanda ya Ziwa walikokabiliwa na mechi mbili za Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar na Biashara United.

Mkude alishindwa kuungana na wenzake kuelekea Bukoba, Jumatano iliyopita tayari kwa mechi dhidi ya Kagera Sugar waliyoshinda kwa mabao 3-0 Uwanja wa Kaitaba, kabla ya juzi kuichapa Biashara United mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Karume, mjini Musoma, Mara.

Mkude alikosekana katika mechi zote mbili, huku ikielezwa kuwa ni baada ya kuchelewa ndege, hivyo kuachwa jijini Dar es Salaam, japo yapo madai kuwa kiungo huyo aliikacha safari hiyo.

Inadaiwa kuwa muda mchache baada wachezaji wa Simba kuondoka Dar es Salaam kwenda Bukona na kubaini hali hiyo itamletea shida, kwa sababu tiketi yake ilikuwa imekatwa, Mkude anadaiwa kuomba kutumia fedha zake kupanda ndege kuwafuata wenzake, lakini aligomewa.

Taarifa ambazo BINGWA imezipata kutoka kwa mtu wa karibu na Mkude, aliyetia ngumu mchezaji huyo asijiunge na wenzake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Senzo Mazingiza.

Ikumbukwe kuwa siku ya mechi na Kagera Sugar, bosi huyo raia wa Afrika Kusini, alipanda ndege alfajiri kwenda kushuhudia mchezo huo na kuzungumza na wachezaji ili kuongeza chachu ya ushindi baada ya kupata fununu za uwepo wa hujuma.

Mtoa taarifa huyo alieleza kuwa kitendo cha Mkude kukosekana katika kikosi, kimemkasirisha bosi huyo ambaye ameahidi kushughulikia suala lake baada ya kurejea Dar es Salaam.

Alisema hata Mkude alipopiga simu kuomba kwenda hata katika mechi na Biasharabaada ya kukosa ile ya Kagera, bado Mazingiza aliendelea kushikilia msimamo wake na kumtaka amsubiri Dar es Salaam.

“Mkude amekiri kosa lake, alisema aliachwa baada ya kupitiwa na usingizi wakati wenzake wanaondoka, lakini amekataliwa kuungana na timu hadi akutane na CEO mpya, wazungumzie ishu yake.

"Bosi naona amekasirishwa sana na kitendo hicho, hii ishu haijaisha kabisa, Mkude anasubiri ni kitu gani ataambiwa na bosi wake, nadhani kuanzia kesho (leo), anaweza kuitwa,” kilisema chanzo hicho.

Alifafanua kuwa kinachomtia hofu Mkude, huenda akasimamishwa kuchezea timu hiyo kwa sababu anaweza kuambiwa ni kawaida yake, ukiangalia timu imecheza na kushinda bila hata uwepo wake.
Muda mwingine tunalalamika timu zetu na national timu haifanyi vizuri na kuwatukana makocha bure tu,ila tunasahau Tz tunawachezaji vilaza sana
 
Maajabu hayaishi duniani. Yaani kuna watu wanatetea huu upuuzi wa Mkude. Bila nidhamu hakuna mafanikio yoyote yanaweza kuapatikana sio shuleni, kazini, kwenye biashara, kwenye mpira, jeshini, n.k. Na nidhamu mbovu kwa Mkude haikuanza leo. Lakini nawalaumu sana viongozi wa zamani wa Simba kwani wao ndio walioilea hii tabia mbaya ya Mkude wakiogopa kumwadhibu eti atahamia Yanga matokeo yake kuna msimu aliwakosesha ubingwa kwa kupotea kambini wakati timu ilikuwa na mechi ngumu na muhimu mikoani kama sikosei ilikuwa Mbeya na Songea.

Mkude huyu huyu juzi juzi katimulia timu ya taifa na Amunike kutokana na nidhamu mbovu. Kwa mtindo huu wa kuendeleza nidhamu mbovu haitakuwa rahisi kwenda kucheza nje ya nchi ataishia hapa hapa bongo. Na mchezaji mwenye nidhamu mbovu asipoadhibiwa kwanza anawambukiza wenzie tabia mbaya pili anashusha morali kwa wenzake. Nafikiri sasa ni wakati muafaka kwa Mkude kupewa adhabu ambayo itamjenga kama kukatwa mshahara, posho ya mechi. n.k. lengo likiwa kumfundisha zaidi nini umuhimu wa nidhamu kwenye timu. Kwa hili viongozi wasilee maradhi hata kidogo.
Tunafail Tz kwasababu za akili hizi mkuu,mtu anatetea ujinga huu
 
Mkuu, bado tu hutaki kuelewa kuwa Simba iko kwenye mabadiliko ya kuachana na Uswahili na kuingia kwenye usasa? Wewe na Mkude wako mnapaswa kulielewa hilo.

Huko Uswahilini waendelee kubaki Vyura FC na jamaa zao wengine. Sisi tumeshakamata kasi kuelekea modern soccer management.
Haya bwana kua uyaone!
 
CEO Yupo sahihi.. mkude anataka kufuata njia ya Balotel, Mkude tunakupenda lakini Simba tunaipenda zaidi kuliko Wewe, usilewe sifa
 
watu wanahujumiana huyo katumwa! Kitanuka sasa hivi kama akichukuliwa hatua!
Kweli kabisa, inawezekana kabana mianya ya kupata hela ya kahawa maana hizi timu kuna watu wanajimilikisha so wanataka kumpigisha shoti, Mkude anatumika tu kuanzisha chokochoko
 
CEO Yupo sahihi.. mkude anataka kufuata njia ya Balotel, Mkude tunakupenda lakini Simba tunaipenda zaidi kuliko Wewe, usilewe sifa
Na huo ndio msimamo wa wanaSimba tulio wengi. Walikuwepo akina Hussein Masha, mchezaji ambaye hakuwahi kukosa penati katika historia ya soka, leo hayupo Msimbazi itakuwa Mkude. SIMBA KWANZA!
 
Mkude kasikia na atajirekebisha, na anaomba radhi kwa yaliyotokea.
Kaahidi Jambo hili kuto jirudia tena.
This is .......mba
 
Nipo pamoja na C.E.O uhuni na uswahili tuwshawaachia chura.
 
Mfukuzeni aje kwenye timu ya wazazi wake..mmenielewa?dirisha dogo bado mwezi kufunguliwa
 
Hizo cheche zilizotemwa ni zipi? Mbona habri yenyewe ni kama story za kijiweni
 
Back
Top Bottom