Nina mtoto wa kiume ana miaka miwili na nusu sasa, anatatizo la cerebral palsy au Autism, (kwa muonekano wa haraka haraka haonyeshi kama ana tatizo hilo) Mpaka sasa hajaweza kusimama au kutembea peke yake mpaka kwa msaada wa kushikiliwa mkono, pia hajaweza kuongea, msaada pekee wa kitabibu tunaopata ni kufanya mazoezi ya viungo (Physiotherapy) kwa muda wa miezi kumi sasa. Lakini maendeleo bado ni kidogo sana. Kuna mtu yeyote anaepitia experience kama hii na je kunaweza kuwa na msaada wa kitabibu zaidi ya mazoezi tunayofanya?