Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Mara Chacha Heche
ameeleza masikitiko yake kufuatia hatua ya Jeshi la Polisi
Kanda maalum ya Dar es Salaam kuwazuia wafuasi wa chama hicho na wananchi kwa ujumla kuhudhuria kesi zinazomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu
Zilizokuwa zimeletwa kwa ajili ya kutajwa na kusikiliza maelezo ya awali Aprili 24.2025, kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi KisutuAkiwa kwenye mahojiano maalum na Jambo TV leo, Jumamosi Aprili 26.2025, Chacha Heche amekanusha madai ya kwamba viongozi na makada wa chama hicho walipanga kuandamana na
'kukinukisha' kwenye viunga vya Mahakama hiyo, badala yake amesema wote waliopanga kufika Mahakamani siku hiyo walikuwa na dhamira njema ya kufuatilia mwenendo wa kesi ya kiongozi wao na si vinginevyo, na kwamba hakuna kosa lolote walilofanya kwa kufanya hivyoChacha Heche ameenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa viongozi na wafuasi wa CHADEMA wataendelea kujitokeza Mahakamani pindi kesi za Tundu Lissu zinapotajwa
John Heche ameenda kubeba watu wa kijijini kwake amewajaza makao makuu ya chadema wanalala hapo na kula hapo kwa gharama za chadema. Akiulizwa anajibu eti ni mashemeji wa Lissu kwa kuwa Lissu kaoa Tarime
John Heche ameenda kubeba watu wa kijijini kwake amewajaza makao makuu ya chadema wanalala hapo na kula hapo kwa gharama za chadema. Akiulizwa anajibu eti ni mashemeji wa Lissu kwa kuwa Lissu kaoa Tarime