Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Katibu wa NEC, Organizesheni wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Chacha, amesema CCM haina ajenda za kuua watu, kama ambavyo Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, John Heche, amekuwa akidai.
Akizungumza jijini Dodoma, Chacha amemnukuu Heche akisema, "Wasira ni mzee anasinzia kwenye vikao, inawezekana ajenda za muhimu sana zikampita, hasa ajenda za kuua watu" Chacha amesema kauli hizo zinapaswa kufuatiliwa na vyombo vya usalama "Je, CCM tuna ajenda za kuua watu? Kwa hiyo vyombo vya usalama mwangalieni yule jamaa.
Maana yake ni kwamba ndani ya CHADEMA kuna ajenda za kuua watu," amesema Chacha. Aidha, amesema CCM haina tatizo na uwepo wa vyama vya upinzani, akieleza kuwa vina nafasi muhimu katika kutoa mawazo mbadala na ya kukinzana katika mfumo wa kidemokrasia. "CCM inahitaji upinzani, haina shida nao kwani tunahitaji mawazo mbadala, mawazo kinzani," amesema Chacha.