Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 677
Habari Zilizoenea Ni Kuwa Waasi Wa Serikali Ya Chad Wakitokea Magharib Mwa Sudan Wameingia Mji Mkuu Wa Chad Ndjamena Na Wanaelekea Ikulu Na Rais Wa Nchi Hiyo Idris Deby Ameshakimbia Nchi.
mvts za rebels zipo www.cnn.com kwa takribani siku tatu sasa........lakini kuna updated report(about 10:22 AM EST) ya kina!!!! kana unataka tinga hapo cnn.com
Jamaa wamekatiza jangwa na mapick up yao wakitokea Sudan, baadhi ya witnesses walioko Hotel Le Meridien wanasema baadhi ya wananchi waliwakaribisha rebels kwa shangwe, sasa I guess baadhi ya wananchi washachoka na utawala wa Deby.
400 rebels wako mjini na hawataki mchezo . Wacha tuangalie . Ama kweli watawala wa Africa sijui wana laana gani . Yaani wanasoma Ulaya na kuishi huko ila wakirudi huwa hawajui ama wanasahau yale waliyo yaona ugenini .Balozi wao sasa anawaita wale ni Terrorists baada ya kumwaga mabovu nyumba ya Balozi wa Saudi Arabia . Nadhani Saudi Arabia watakuwa wameshiriki uozo so wana wamwagia nyongo na tindikali .
Wapiganaji nchini Chad wameingia mji mkuu Ndjamena na kuiteka Ikulu ya rais huku taarifa zikisema kumekuwa na makabiliano makali kati ya waasi na majeshi. Walioshuhudia wamezungumzia kuona magari ya majeshi yakiteketea barabarani.
Hata hivyo Waziri wa maswala ya kigeni wa nchi hiyo amesema Rais Deby yu salama na hali katika mji huo imedhibitiwa. Mwenzake wa Ufaransa ambayo imekuwa ikiunga mkono upande wa serikali ameshutumu hatua hiyo ya waasi kujaribu kutwaa mamlaka.
Alidai kwamba kuna mwingilio wa kijeshi kutoka nje.
Muungano wa Afrika. Inaaminika wapiganaji hao walianzia maasi yao katika mpaka wa Chad wa mashariki ulio karibu na Sudan mapema juma hili. Serikali ya Chad imekuwa ikilaumu Sudan kwa kuunga mkono wapiganaji hao na Sudan nayo ikiishutumu Chad kwa kuunga mkono waasi huko Darfur.
Ufaransa imewataka raia wake wote walioko Chad kutotoka nje.
Muungano wa Afrika umetaka waasi hao wasitishe harakati zao na kuonya kwamba iwapo waasi watatwaa mamlaka Chad itafukuzwa kutoka kwa muungano huo.