Chad Yaachana na ICC kwa Madai ya Ubaguzi dhidi ya Mataifa ya Afrika

Chad Yaachana na ICC kwa Madai ya Ubaguzi dhidi ya Mataifa ya Afrika

Kadhakan

Senior Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
126
Reaction score
201
Serikali ya Chad imetangaza mpango wa kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), ikidai kuwa chombo hicho cha kusimamia sheria kimekuwa kikionesha ubaguzi dhidi ya mataifa ya Afrika katika utekelezaji wa majukumu yake.
Screenshot_20260728-120713.png


Katika taarifa iliyotolewa Julai 27, 2026, serikali ya Chad ilisema uamuzi huo umetokana na kile ilichokiita ukosefu wa usawa katika uendeshaji wa mashauri ya ICC. Ilieleza kuwa kati ya mashauri 13 yaliyofunguliwa tangu mahakama hiyo ianze kazi mwaka 2002, tisa yanahusu mataifa ya Afrika.

soma zaidi:ICC Yaanza Mchakato wa Kuamua hatma ya Muendesha Mashtaka Mkuu Karim Khan

Kwa mujibu wa serikali hiyo, hali hiyo imeibua maswali kuhusu usawa na uadilifu wa ICC. Pia imezitaka nchi za Afrika kuendelea kuimarisha mifumo yao ya sheria za ndani ili kushughulikia makosa makubwa badala ya kutegemea mahakama za kimataifa.

Hatua ya Chad inaifanya ijiunge na Burkina Faso, Mali na Niger, ambazo pia zimeanza mchakato wa kujiondoa ICC. Nchi hizo zimekuwa zikiikosoa mahakama hiyo kwa madai ya ubaguzi wa kijiografia na kutowajibisha viongozi wa mataifa mengine kwa kiwango sawa.

ICC, yenye makao makuu mjini The Hague, Uholanzi, ilianzishwa kwa lengo la kuwafikisha mbele ya sheria watu binafsi wanaotuhumiwa kwa makosa makubwa ya kimataifa, ikiwemo uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya kimbari, pale ambapo mifumo ya sheria ya kitaifa imeshindwa au haitaki kuchukua hatua.
 
Hiyo ICC ni kituko Tu, ina double standard, kama ni Haki basi iwe Kwa wote hata mataifa makubwa na viongozi wake.
 
Back
Top Bottom