Pre GE2025 CHADEMA, ACT Wazalendo na CUF tengenezeni Alliance kupelekea uchaguzi 2025

Pre GE2025 CHADEMA, ACT Wazalendo na CUF tengenezeni Alliance kupelekea uchaguzi 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
20,189
Reaction score
29,663
Nilichokiona kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa ni kwamba wananchi Wana muamko wa kupigia kura upinzani shida upinzani umegawanyika.

Nina shauri ya kwamba upinzani wafikirie kutengeneza alliance ambapo wataungana 2025 na kuwa na mgombea mmoja wa urais, ubunge na udiwani kwa kuangalia chama gani kinakubalika kwa eneo.

2025 msimame pamoja kwa Hila za CCM kila chama kikisimama chenyewe hakuna litakalopatikana.
 
Hata vikiungana vyama vyote vya Afrika nzima haviwezi kuiondoa CCM.
Kitu pekee cha kuiondoa CCM ni kubadilisha mfumo wote wa kiutawala nchini,kitu ambacho ni kigumu kwa kuwa wanaoshikilia huo mfumo ni wao wenyewe.
Njia nyingine iliyopo ni watu kwenda front kwa njia ya Upanga-kitu ambacho napo ni kigumu kwa kuwa Nyerere aliwaongoza watu kwa njia ya hofu na uoga-watu wamekuwa wakirithishana vizazi. A vizazi.

Njia pekee ni kuomba CCM wawe wanachagua viongozi aina ya Magufuli-kitu ambacho hawatakuja kurudia hilo kosa tena.
So,tusubiri miujiza.
 
Umeongea kweli. Lakini wakiungana Kuna nguvu watajenga ya kuitikisa system na kubadilisha kwa njia ya katiba Mpya.
 
chadema walisha chemsha toka 2015 itawachukua miaka 60 kurudi pale walipofika kwa wakati ule, huku wakiachwa mbele miaka 160 na chama cha mapinduzi
 
wakiacha umimi na uroho wa madaraka muungano wao utakuwa ni wenye nguvu sana, rejea jimbo alilogombea mtatiro wakati ule wa jiwe.
 
CCM mnataka wepesi tena kama mlivyoumaliza UKAWA dakika za majeruhi - mzee wa CUF eti nafsi imenisuta ha ha ha
Mzee mwingine na yeye akagomea kwake chumbani hatoki.. Njaa hizi za uzeeni...balaa.

Nchii hii ina mazingaombwe mengi sana.
 
Huo muungano utakuwa ni sawa na UKAWA. Kwa CCM hii hautafua dafu, humo humo kutakuwa na usaliti miongoni mwa viongozi wake. Labda huo muungano usihusishe CHADEMA. CHADEMA ni chama kikubwa kinatosha kushindana chenyewe bila muungano wa vyama vingine
 
Unamaanisha Mbowe, Lipumba na Zitto wapambane kutoa CCM madarakani! You can't be serious!
 
Vyama vya siasa vikikomaa na katiba mpya lazima waachie serikali,maana kinachowapa nguvu ni katiba mbovu iliyopo.
 
Nilichokiona kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa ni kwamba wananchi Wana muamko wa kupigia kura upinzani shida upinzani umegawanyika.

Nina shauri ya kwamba upinzani wafikirie kutengeneza alliance ambapo wataungana 2025 na kuwa na mgombea mmoja wa urais, ubunge na udiwani kwa kuangalia chama gani kinakubalika kwa eneo.

2025 msimame pamoja kwa Hila za CCM kila chama kikisimama chenyewe hakuna litakalopatikana.
Hata waungane wote, bila Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Katiba Mpya hakuna kitu ni wizi wizi tu. Polisi, wakurugenzi na watendaji watenganishwe na mambo ya uchaguzi. Huwezi kuwa mchezaji na refa kwa wakati mmoja.
 
Nilichokiona kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa ni kwamba wananchi Wana muamko wa kupigia kura upinzani shida upinzani umegawanyika.

Nina shauri ya kwamba upinzani wafikirie kutengeneza alliance ambapo wataungana 2025 na kuwa na mgombea mmoja wa urais, ubunge na udiwani kwa kuangalia chama gani kinakubalika kwa eneo.

2025 msimame pamoja kwa Hila za CCM kila chama kikisimama chenyewe hakuna litakalopatikana.
waipe jina la Second Failed Alliance (SFA) after UKAWA na itapendeza zaid gentleman 🐒
 
Hivi unataka chama kikubwa kama chadema kiungane na chama kipi hapa bara?
1. ACT yenye wanachama Kigoma mjini pekee?
2. ADC, SAU CHAUMA, TADEA, CUF, NCCR, NLD, DP, n.k. Vyama vya kwenye briefcase na machawa wa ccm?

Chadema Ina mtandao mkubwa sana wa wanachama na Ina uwezo wa kuchukua kiti cha urais endapo tume ya uchaguzi itakuwa huru.

Sasa tume huru inapatikanaje? Hiki ndicho cha kujadili.
 
Hata Wapinzani wa Dunia nzima waungane kwa mtindo huu wa ccm wa kuwafanyia figisu wapinzani na kujitangazia matokeo kadri wapendavyo wakisaidiwa na majeshi yote wapinzani hawatoboi.
Njia pekee ambayo inaweza kuwatoa madarakani ni ile waliyotumia Waarabu wa kaskazini mwa Afrika kufanya maandamano yasiyokoma hadi wenyewe watoroke nchi,njia ambayo Watanzania na ukunguru wetu huu tulio nao hatuthubutu.
 
Back
Top Bottom