CHADEMA amsheni watu kwa kauli za kina Chalamila kwa mjamzito kwamba kama hatoi Shs 50,000 arudi nyumbani mume wake amkate kwa kisu na mkasi ajifungue

Unfortunately Mkuu, hiyo ndio reality ambayo watu kama Chalamila wanapaswa kuitambua. Angalia pale kazini, ofisini nk. Nani wana watoto wengi? Sasa kujifanya huoni kwamba jamii ya Watanzania haijaelimika bado kufikia huko ni kuwa kiongozi mbovu. Lazima tukiri kwamba bado ujinga katika masuala ya kupanga uzazi ni tatizo nchini, na hatuwezi kuwafundisha watu kwa kuwakomoa.

Hebu niambie, kuna harusi umewahi kwenda ambayo waalikwa hawatarajii mke kuwa mjamzito ndani ya miezi tisa? Hiyo itakuambia mentality ya Watanzania iko wapi. Wanahitaji kuelimishwa sio kukomolewa. Unapochukua jukumu la uongozi huo unakuwa wajibu wako, sio kuwajibu watu utumbo
 
Ameongea vizuri tu.Ni mapokezi na tafsiri ya maneno.Mkiwapa wake wenu ujauzito muwaandalie vifaa na fedha za dharula.Rahisi tu.Dezodezo hakuna.Kipi kigumu kuelewa?
Wewe utakuwa bikira bado. Wanaume wangapi wakipewa mbususu wanauliza vipi ukipata mimba kabla ya kuichangamkia?
 
Wewe utakuwa bikira bado. Wanaume wangapi wakipewa mbususu wanauliza vipi ukipata mimba kabla ya kuichangamkia?
Bikira mwenye dushe,ndevu na miaka 45+ jumlisha mke na watoto watano?Nasisitiza;Hakuna vya bure!Jiandaeni kwa kuhudumia mahawara na wake wenu/ndugu zenu.Kwisha.
 
Hamna dada yako, binamu yako au ndugu yako yeyote aliewahi kudungwa mimba bila kupanga? Kumbuka ni wanyama tu wanao mate kwa lengo la kuzaa, sio wanadamu. Huenda hata mimba yako haikupangwa pia.
Mimba yangu ilipangwa la sivyo ningepata utapia mlo?

Mfano ukidungwa mimba Leo bahati mbaya una miezi Tisa ya kujiandaa
 
Bikira mwenye dushe,ndevu na miaka 45+ jumlisha mke na watoto watano?Nasisitiza;Hakuna vya bure!Jiandaeni kwa kuhudumia mahawara na wake wenu/ndugu zenu.Kwisha.
Usisahau kuwa si wanaume wanaoenda kujifungua hospitali. Idadi ya wenye mimba walionunuliwa chips kuku wakatoa mbususu na kutelekezwa walipopata mimba ni kubwa mno. Wengine ni watoto wadogo tu. Na kati ya hao watoto wako watano usije shangaa siku moja anatokea mwenye kupata mimba wakati hana uwezo bado wa kujihudumia. Zaidi ya 40% ya mimba zinazotengenezwa zinakuwa hazikukusudiwa kuwa mimba, na 70% ya hizo mimba wanaume waliozisababisha wanaingia mitini.
 
Mimba yangu ilipangwa la sivyo ningepata utapia mlo?

Mfano ukidungwa mimba Leo bahati mbaya una miezi Tisa ya kujiandaa
Ongea reality ya Tanzania Mkuu, hapa sio Norway au Sweden. Tuna kesi nyingi tu za watoto kutupwa chooni, mitaroni nk, na sababu zinajulikana.

Chalamila anaongea utafikiri kila Mtanzania ana kipato cha Tshs 500,000 kwa mwezi.
 
Huyu jamaa Yuko miongoni mwa watu ninaowapuuza,ni bure kabisa,Kwa uzoefu wangu ukikutana na mtu mwenye bichwa ka la huyo bwana jua kichwani hakuna kitu,Kuna maziw Mgando tu.
 
Ongea reality ya Tanzania Mkuu, hapa sio Norway au Sweden. Tuna kesi nyingi tu za watoto kutupwa chooni, mitaroni nk, na sababu zinajulikana.

Chalamila anaongea utafikiri kila Mtanzania ana kipato cha Tshs 500,000 kwa mwezi.
Basi serikali ikigharamia 5000 ya groves harafu mtoto atakupwa si hasara hiyo Sasa inabidi watanzania wakumbushwe kwamba uzazi na malezi ni gharama

Harafu wewe inaonekana unazungumzia Tanzania ya enzi za mwalimu
 
Nilitegemea uwe mstaarabu na kunitaka radhi kwanza kwa kunifananisha jinsi iso yangu.Na ndiyo maana mnashauriwa na JF kuitana "wakuu" na siyo majina mama,dada,babu,mke ,shangazi nk.
Anyway,sina mtoto anayetarajia kwenda labor.Na ninasisotiza;Hao mabinti/wanawake wanaopata mimba kwa namna ulizozoeleza hawaishi kikiwa.Wana ndugu jamaa na marafiki.MuwasIdie kujiandaa.Uelewe tu,hakuna dezo dunia hii ya leo.Na muwalee kwa maadili mema na kujitunza.Sidhani kama ninalo la kukuongezea.
 
Hilo utajua wewe kama uliletwa duniani bila mipango walaumu wazazi wako na sio serikali
Mkuu wewe ungetaka serikali ifanye jambo gani muhimu kwa wananchi wanaolipa kodi? Au zile nchi ambazo serikali yao wanatoa huduma zote za afya na elimu bure kwa wananchi ni wajinga?
 
Basi serikali ikigharamia 5000 ya groves harafu mtoto atakupwa si hasara hiyo Sasa inabidi watanzania wakumbushwe kwamba uzazi na malezi ni gharama

Harafu wewe inaonekana unazungumzia Tanzania ya enzi za mwalimu
Kama Tanzania ya enzi ya Nyerere ingekuwa imebadilika, CCM wasingeshinda uchaguzi hata siku moja!

Usiangalie flyover, Mwendokasi na majumba ya watu kule Mbweni hapa Dar na watu wanaendesha Toyota Crowns ukadhani Tanzania ya leo imebadilika. Bado sana - na huenda katika ujinga, maradhi na umasikini, ujinga na umasikini vimekuwa hata zaidi ya enzi za Nyerere kwa asilimia kubwa ya wananchi, kwa sababu enzi hizo hawakulipia dawa hospitalini wala karo za shule!

Umewahi kujiuliza kwa nini leo serikali inakusanya kodi kubwa sana lakini huduma kwa wananchi karibu zote zinachangiwa na ni mbovu kuliko enzi za Nyerere? Sio kwa sababu serikali inagharamia huduma nyingi za wananchi - hapana!

Jiulize, ikiwa katika kilalita ya mafuta petroli na dizeli unachangia gharama za kurekebisha barabara zisiwe na mashimo nk, kwa nini barabara zina mashimo kuliko hata kabla ya kuanza kuchangia ukarabati wake? Pesa za kuziba mashimo tunazochangia kila siku zinaenda wapi?

Wewe si uliambiwa tozo za miamala ya simu na vocha zitatengeneza zahanati na barabara za vijijini kwa hiyo toeni Watanzania toeni kodi ya uzalendo. Leo hii huko kijijini kwako mmetenegenzewa barabara ngapi, kuchonga tu?

Kwa taarifa yako tu,siku hela ya tozo ilipoonekana kubwa, bajeti ya magari ya serkali hizi Landcruiser iliongezwa, na wanajeshi wastaafu wakapewa zawadi, maraisi wastaafu na wake zao wakaambiwa watapewa landcruiser mpya kila miaka mitano, nk. Huoni haya madudu yalivyo mengi barabarani siku hizi, unafiiri ni hela ya dhahabu ya Barrick hiyo? Ni tozo unazokamuliwa!
 
Basi huitambui reality ya maisha ya majority ya Watanzania, kama tu Chalamila. Na suala la kukutaka radhi kwa kukufananisha jinsia isiyo yako wala hata sielewi linaingiaje hapa - labda kama unadhani neno bikira halitumiki kwa wanaume!
 
Akili ni ya mtu hapaswi kushikiwa na CHADEMA , ina maana watanzania ni wajinga kiasi kwamba lazima CHADEMA waseme ndo watafunguka akili?


Britanicca nikiwa hapa Albania leo
 
Basi huitambui reality ya maisha ya majority ya Watanzania, kama tu Chalamila. Na suala la kukutaka radhi kwa kukufananisha jinsia isiyo yako wala hata sielewi linaingiaje hapa - labda kama unadhani neno bikira halitumiki kwa wanaume!
Sawa bikira kaka sindezaiza.Have a good day.Tchao!
 
Mkuu wewe ungetaka serikali ifanye jambo gani muhimu kwa wananchi wanaolipa kodi? Au zile nchi ambazo serikali yao wanatoa huduma zote za afya na elimu bure kwa wananchi ni wajinga?
Kama mtu Hana uwezo wa kulipa elfu Tano ya groves ana uwezo wa kulipa kodi gani?

Kitu ambacho hujui kodi inatokana na wananchi na Kwa Tanzania watu wanaolipa direct tax hawafiki million 2 Sasa unataka watanzania million 2 wabebe mzigo wa watanzania million 68?
 
Heee, Watanzania wanaojifungua ni milioni 68?

Kwani unafikiri nchi hii inaendeshwa kwa kodi za Watanzania milioni 2 tu? Watu hamuelewi haya mambo lakini mnapenda kuyasema. Sasa ni hivi, hao milioni 2 ni wale tu wanaolipa kodi kwa P.A.Y.E. Kodi inayoendesha nchi sio PAYE peke yake. Kwa mfano, Watanzania wangapi wanalipakodi kupitia miamala ya simu? Vodocom peke yake wanao zaidi ya milioni 6. Bado Togo sijui nk

Na labda nikuulize, yale mabasi ya CCM yaliyonunuliwa kwa ajili ya Mkutano wa Dodoma ambapo kwa sasa yame park, unajua zile ni gloves za kina mama wanaojifungua nchi nzima kwa miaka mingapi? Unafikiri ni hela ya michango au ruzuku ya CCM zile? Wewe endelea kulala uendelee kuliwa.
 
Wamechoka na matukio ikiwa slaa anaoza mahabusu wana lipi hao jamaa zako wanataka kuchanga harambee kumnunulia chairman lissu v8 200 hilo ndio tukio!
 
Wakina mama wote Tanzania waungane wamkatae Samia Oktoba 2025 kwenye sanduku la kura maana ccm wameshindwa kuboresha huduma za afya.
 
Hata kama tunao waibu wa kuchangia gharama za afya, lakini si kwa kauli hizo za kiongozi..!
Tusimshange Chalamila lakini, nakumbuka alishawahi kuwaambia watu wa Mwanza Samia anakuja ziara ukitaka kumwandikia ujumbe wowote kwenye bango ruksa, hata kama ni matusi!

Niliandaa bango langu la kusema "Samia Nayapenda Macho yako Marembo" watu wakaniambia wee, unamjua muwewe alivo mkali! Sikulipeleka bwana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…