Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
- Thread starter
-
- #81
Umeona eeh? Zipo nyingi sana kauli mtaji toka CCM lakini hawazitumii. Yaani sijui niombe kazi ya kuwa consultant wao wa propaganda, maana kuna kauli nyingi sana za CCM wanajiua wenyewe, kuwahemusha wananchi ni rahisi sana!Chadema kitengo Cha propaganda kimekufa hizi kauli ni mtaji mkubwa kisiasa.
Hauna uelewa mpana kuhusiana na neno kodi. Japo umenisikitisha kiasi, kwamba serikali iwachaji wananchi wake pesa ya gloves? Au wewe unashauri wananchi waache kuzaa then nchi ikose rasilimali watu?Kama mtu Hana uwezo wa kulipa elfu Tano ya groves ana uwezo wa kulipa kodi gani?
Kitu ambacho hujui kodi inatokana na wananchi na Kwa Tanzania watu wanaolipa direct tax hawafiki million 2 Sasa unataka watanzania million 2 wabebe mzigo wa watanzania million 68?
Zaa kama unaweza kulea mkuu usije zaa panyarodi, vibaka na dada poa wakaanza kuongeza mzigo Kwa serikali kuajiri policeHauna uelewa mpana kuhusiana na neno kodi. Japo umenisikitisha kiasi, kwamba serikali iwachaji wananchi wake pesa ya gloves? Au wewe unashauri wananchi waache kuzaa then nchi ikose rasilimali watu?
We ndio hakuna unacho jua qualified keybord worriorBasi hujui siasa wewe.
Well Noted MkuuHao watu ni wajinga kiasi gani hadi wasubiri kuamshwa na chadema, kwanini hawaamki wenyewe?
Jambo moja nililoona kuhusu Chadema ni kwamba mnashindwa kutumia matukio ya kila siku kuwafunua macho wananchi kwa nini serikali ya CCM haipo madarakani kwa faida yao. Hii ni pamoja na matumizi ya kifahari ya fedha ya hivi karibuni ya Mkutano Mkuu wa CCM na kadhalika.
Lakini pale ambapo inatokea viongozi wateuliwa wa CCM kama Chalamila wanatoa kauli za kubeza wananchi, kwa mfano huyu mama aliempigia simu Chalamila kusema analazimishwa kutoa Tshs 50,000 ili wamhudumie kujifungua, halafu Chalamila anamjibu kama hhutaki kutoa hiyo hela chukua bajaji nenda nyumbani kwako mwambie mumeo achukue kisu na mkasi akutoe mtoto, hizo ni kauli zilizokosa staha, zenye kuonyesha kiburi na majivuno ya uongozi wa CCM kwa wananchi wake.
Sababu ni kwamba Watanzania tunatozwa kodi katika maeneo mengi sana, lakini fedha hizi za kodi zetu zinaonekana kuwanufaisha watu wachache kama kina Chalamila katika matumizi yao ya anasa kutia ndani na mambilioni wanayotumia kama posho, kununua magari ya kifahari nk. Na hata kama wananchi, pamoja na mlolongo wa kodi wanazokatwa, wanatakiwa kuchangia gharama za hospitali, wananchi wanapohoji kitu lazima ajibiwe kwa heshima na ustaarabu.
Tumuulize Chalamila; jibu alilompta huyu mama linaendama na imani ya CCM kwamba kila mtu anastahili heshima? Au huo ndio msimamo wa Raisi Samia ambaye nae ni mwanamke anaejua maana ya kujifungua? Vipi wakati Samia akijifungua mwanae Abdul angepewa jibu la namna hii na mkuu wa mkoa wa wakati huo?
Huduma za kujifungua ni mojawapo ya huduma dharula ambazo hazipaswi kuwekewa masharti ya leta hiki na kile kabla hatujakuhudumia. Hizi tozo nyingi mnazotutoza elekezeni huko badala ya kujibadilishia magari makubwa ya serikali kila baada ya miaka mitatu.
Inafikia mahali viongozi wa CCM wanawaita wananchi wasio na uwezo ni wazembe? Hawajui tena shida za wananchi kwa sababu wao wana hela za ufisadi?
Ni wazi hawa watu wa CCM wamelewa madaraka na kujiamini kwamba hata wakiwatukana wanachi na kuwakebehi, wataendelea kuwa madarakani. Chadema, vitu kama hivi vitumieni kuwaamsha wananchi juu ya ukweli wa aina ya watu wanaojiita viongozi wao
View attachment 3214787
Angalia pia: https://www.jamiiforums.com/data/video/5941/5941542-128f28144764987ee2bf3cd653521c1d.mp4
Yaani mtu yupo Dar es salaam hapa hapa anataka kujifungulia bure?Elfu 50 sio elfu tano. Watanzania wengi sana bado hawana elimu ya kutambua ukiwa huna uwezo usizae sana au usizae kabisa - bado wanaishi kwa filosofia kwamba kila mtoto anakuja na baraka zake. Kwa hiyo viongozi wanapaswa kuchululia level yao ya kuelimika into context.
Mbona wanafurahia u-semi illiteracy wao wa kisiasa kwenye kupiga kura?
Katoka hadharani lakini badala ya kuomba radhi kajikanganya katika maelezo yake na kukanusha akieleza kuwa kanukuliwa vibaya na vyomba vya habari. Hayo aliyoyasema hapo awali akiwa mubashara kabisa tumeyaona na kuyasikia. Waandishi wa habari hawakunukuu aliyoyasema bali yote mwenyewe anaonekana akiyaongea hayo maneno yake na suala la kunukuliwa vibaya halipo. Muungwana haropoki na akivuliwa nguo huchutama. Huyu jamaa badala ya kuchutama kaendelea kusimama na kuacha vitu vyake hadharani.Chalamila aonywe ameteleza ila ni Kiongozi mzuri.Atoke Hadharani aombe radhi.
Huyu hafikirii, anakariri neno nimenukuliwa vibaya, eti wrong context. Hili sio suala la kumnukuu, bali la kumsikiliza! Watu wamereact kutokana na kitu walichosikia toka mdomonimwake sio walichosoma kilichoandikwa na waandishi wa habari!Katoka hadharani lakini badala ya kuomba radhi kajikanganya katika maelezo yake na kukanusha akieleza kuwa kanukuliwa vibaya na vyomba vya habari. Hayo aliyoyasema hapo awali akiwa mubashara kabisa tumeyaona na kuyasikia. Waandishi wa habari hawakunukuu aliyoyasema bali yote mwenyewe anaonekana akiyaongea hayo maneno yake na suala la kunukuliwa vibaya halipo. Muungwana haropoki na akivuliwa nguo huchutama. Huyu jamaa badala ya kuchutama kaendelea kusimama na kuacha vitu vyake hadharani.
Mkutano wa nishati ukiisha naye afurushwe kwenye ofisi za Umma, hafai kuwa kiongozi wa wananchi.Mungu saidia huyu baba atumbuliwe