urithiwetu
Senior Member
- Mar 5, 2009
- 103
- 3
- Waende wasiende haiongezi wala kubadili anything, dawa ni ku-do away na vyama vyote vya siasa bongo tuanze upya!
Respect.
FMES!
Mimi naamini hakuna sababu ya kuunganisha vyama. Unapofanya hivyo ccm nayo inafanya bidii kujiingiza katika huo ushirikiano ambao baadae hauwi tena ushirika mtakatifu.
Lakini vyama vikijipanga vyenyewe vyema, wananchi watachagua vyama vilivyo bora. Mfano, tizama yaliyofanyika kiteto, busanda, magogoni, tarime n.k
Respect mkuu,- Hebu rudia tena una maana gani sijakuelewa bado? Kwamba kuna watu watakwenda kumpigia kura Nchimbi, sasa what this has to do na mawazo yangu na mimi FMES?
Respect.
FMEs!
Mzee Mwanakijiji
Ongezea na hizi:
1. Aidha wajifunze ustaarabu, manati hazileti ushnindi
2. Kama mgombea kiti cha urais ni Mh. Mbowe, wasahau kabisa kushika dola. Bisha nikupe sababu.
Kubalini tu mmeshindwa Busanda ndiyo maana hamkutaka kutokea wakati wa kutangaza matokeo kwa kuogopa aibu. Mlikuwa na vijana wengi wa kijiweni tu ambao mliwalipa Shs. 500/- za kazi ya kuzomea lakini mkakosa wapiga kura vijijini. Ama kweli mikakati ya uchaguzi hamna kabisa.
Mambo ya mahesabu nayo ni fani na yanawenyewe..- Now my point is, Ninasema panga pangua, bungeni kutakua na at least wabunge CCM 60% kwa 50% upinzani kwenye uchaguzi wa kwanza, unaofuatia CCM itaondoka,
Respect.
FMES!
Well.. I still stand on my initial suggestions..
They are wasting time, money and talent.
They are wasting time, money and talent.
Mkjj,
Nadhani wakati ulipotoa ushauri huu wengi hawakukuelewa au waliamua kudharau na kutokuchukua hatua za makusudi za walau kufanya utafiti wa nini ulichoandika. Mimi si mpenzi wa CHADEMA lakini matokeo yanapotoka katika chaguzi hizi kuna haja ya kufanya postmoterm na kubaini makosa na mambo mengine.
Je, inawezekana kuwa kwa vyama hivi vya siasa kushiriki katika chaguzi hizi bila ya kujali kushinda ama kushindwa, kuna manufaa yeyote ambayo hupatikana kwa kikundi cha watu au mtu mmoja mmoja kwa njia yeyote ile ama iwe ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, nk?
Kushiriki katika huu uchaguzi kumekijenga sana Chadema. Wezi wa kura wameshinda, lakini Chadema imefahamika na kupendwa zaidi. Kushiriki kulikuwa na faida kubwa, na sio hasara.
Inachekesha mtu kuiba na kukuambia fuata sheria (za kwenda mahakamani). Yeye mbona hafuati sheria?
Hakuna kitu kinachotishia usalama wa taifa la Tanzania kwa kasi zaidi kuliko uchu wa madaraka wa CCM. Hawa wanahodhi madaraka kwa kuiba kura za wananchi. Wanahatarisha sana amani yetu.
Usalama wa taifa tayari uko mashakani, ustawi wa jamii umeporwa uwajibikaji umekimbia na uungwana hakuna tena.Kushiriki katika huu uchaguzi kumekijenga sana Chadema. Wezi wa kura wameshinda, lakini Chadema imefahamika na kupendwa zaidi. Kushiriki kulikuwa na faida kubwa, na sio hasara.
Inachekesha mtu kuiba na kukuambia fuata sheria (za kwenda mahakamani). Yeye mbona hafuati sheria?
Hakuna kitu kinachotishia usalama wa taifa la Tanzania kwa kasi zaidi kuliko uchu wa madaraka wa CCM. Hawa wanahodhi madaraka kwa kuiba kura za wananchi. Wanahatarisha sana amani yetu.
Mwanakijiji..Pundamilia, hakuna kitu kibaya kama kiburi cha madaraka (the arrogance of power). Jinsi ambavyo CCM haisikii masahihisho ambayo watu walio nje wanayaona (wanasema chama ni safi ila mtu mmoja mmoja siyo safi). Kiburi hiki hiki ndicho ninakiona Chadema vile vile. Lakini chao ni tofauti na cha CCM. Wao CCM ni kile kiburi kinachotokana na kutawala wakati kile cha Chadema kinatokana na kukubalika na umaarufu wake katika vita ya ufisadi. Kiburi hicho hicho kinaonekana CUF kwa namna tofauti (ngome yao ni Pemba na Zanzibar kwa jumla na hivyo hawako tayari kupanua wigo wao).
Chadema sifikirii kama inaweza kubadillika na kujiandaa kuwa chama tawala kwa kadiri ya kwamba kinaendelea kufanya yale yale kikitarajia mambo tofauti. Kuna mtu itabidi awaambie ukweli utokanao na urafiki.
Hata mimi naona Chadema imepata sympathy kubwa kuliko kama kisingeenda kule; ungekuwa ndio mwisho wake maana kingeonekana hakina mtandao wa ki-nchi- so now cha mhimu ni chadema; dk slaa; mbowe; zitto itisheni; tundu lisu; mikutano mfululizo dar- na mikoani kuelezea kilichotokea kiteto-tarime ( ingawa mlishinda)-mbeya vijijini-busanda-na biharamulo; nguzo yenu iwe ktk ufisadi muonyeshe dhamira ya dhati; usawa na kutaka kupata utawala usio na damu; wizi wa kura na ubovu wa NEC na umhimu wa mabadiliko ya dhati; uzuri wa chadema na kunawirisha kiasi sera zenu( hata ktk website); wekeni wazi ni chama cha wanachama na watanzania; jiandae kwa uchaguzi wenu kwa demokrasia safi; jiandaeni kwa uchaguzi serikali za mitaa; naamini mna nafasi nzuri- pia wekeni wazi watu wa kada tofauti wawachangie sasa maana hiyo ndio ownership ya chama na muwe wazi ktk matumizi; INAWEZEKANA-INAWEZEKANA-INAWEZEKANA TZ BILA CCM
Pundamilia, hakuna kitu kibaya kama kiburi cha madaraka (the arrogance of power). Jinsi ambavyo CCM haisikii masahihisho ambayo watu walio nje wanayaona (wanasema chama ni safi ila mtu mmoja mmoja siyo safi). Kiburi hiki hiki ndicho ninakiona Chadema vile vile. Lakini chao ni tofauti na cha CCM. Wao CCM ni kile kiburi kinachotokana na kutawala wakati kile cha Chadema kinatokana na kukubalika na umaarufu wake katika vita ya ufisadi. Kiburi hicho hicho kinaonekana CUF kwa namna tofauti (ngome yao ni Pemba na Zanzibar kwa jumla na hivyo hawako tayari kupanua wigo wao).
Chadema sifikirii kama inaweza kubadillika na kujiandaa kuwa chama tawala kwa kadiri ya kwamba kinaendelea kufanya yale yale kikitarajia mambo tofauti. Kuna mtu itabidi awaambie ukweli utokanao na urafiki.