Kushiriki katika huu uchaguzi kumekijenga sana Chadema. Wezi wa kura wameshinda, lakini Chadema imefahamika na kupendwa zaidi. Kushiriki kulikuwa na faida kubwa, na sio hasara.
Inachekesha mtu kuiba na kukuambia fuata sheria (za kwenda mahakamani). Yeye mbona hafuati sheria?
Hakuna kitu kinachotishia usalama wa taifa la Tanzania kwa kasi zaidi kuliko uchu wa madaraka wa CCM. Hawa wanahodhi madaraka kwa kuiba kura za wananchi. Wanahatarisha sana amani yetu.
Usalama wa taifa tayari uko mashakani, ustawi wa jamii umeporwa uwajibikaji umekimbia na uungwana hakuna tena.
Nini wananchi wategemee, swala la kulalamika kuhusu ufisadi na kufikiri serikali ya CCM itashughulikia wizi na udanganyifu ni kupoteza muda. Unayetaka awashughulikie mafisadi yeye mwenyewe anatumia wizi na hila kuingia madarakani sasa kiko wapi.
Swala la Chadema kutoshiriki uchaguzi hilo siliafiki, Hata Obama aliaambiwa muda bado asigombee, weusi South Afreka waliaambia hawajui kutawala, Uhuru wetu tuliambiwa hatujakomaa kujitawala na hatuna mtandao mzuri, weusi marekani walionekana hata wao hawajijui. Huwezi kujiandaa kisiasa au kujikuza kisiasa kwa kukimbia kushindwa au kushindana kisiasa haya yote yanaendana, kipimo kimoja wapo cha kujua hali yako ni pale tu unaposhindana ndipo utajua wapi unamatatizo.
Nawashauri Chadema waendelee kushiriki kwenye Chaguzi huku tukijijenga kuanzia chini kwenda juu, hapa Chama kilipo ni pazuri sana na sintochelea kumsifia na kumpongeza kila mwana Chadema alikiwezesha chama kufika hapa kilipo hii ni hatua kubwa tena ya kujivunia, kwani ni lini tulitegemea CCM wangeamua kulala macha kwa ajili ya kuogopa upinzani leo wanaiba mchana kesho wataona haya.
Mwanakijiji mawazo yako yanaweza kuwa mazuri ila hatari sana hasa kwenye ushindani wa siasa. Mwaka 1992 hakuna chama cha upinzani kilichokuwa na mwanachama hata mmoja wangesema wasubiri kwa woga mpaka leo tusingekuwa hata na diwani, si haba tumepata chama walau kutoa duku duku zetu, ni wajibu wetu kuungana na wanaharakati wenzetu na kuongeza nguvu, je kama wanajambo wote wenye mapenzi mema wangekuwa Chadema leo wizi ungepungua kwa asilimia nyingi sana.Tujipange tukiwa mstari wa mbele sio kuweka silaha chini, tutapoteza hata tulichokomboa.
Hongera Chadema, Hongereni wote mnaopigania demokrasia hii vita ni ngumu na ya muda mrefu ila tutashinda, tunaweza, tuna nguvu na tunajivunia nchi yetu. Ndio tutashinda tena kwa kishindo.