CHADEMA: Baada ya Biharamulo; Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010

Kitakachoiokoa NCHI hii toka mikononi mwa CCM ni pale tu WAGOMBEA HURU watakaporuhusiwa. Bahati mbaya kabisa ruhusa hii inatakiwa itolewe na SERIKALI ya CCM. Kwa sasa tuendelee tu na hizi blah blah za kuitaka CHADEMA, CUF, TLP,...wafanye hiki; waache kile;
Tatizo letu ni KATIBA.
 
Mkuu Mkandara,
Nashukuru sana kwa ushauri wako,humu ndani ya JF ni miongoni mwa watu nikiona mabandiko yao huwa sisiti kuyasoma ya wengine nayaruka.Hilo pendekezo lako ni zuri sana na Wanachadema na wapenda demokrasia wote wanalikubali.
Ugumu upo kwenye utekelezaji viongozi wa CHADEMA kwa upande wao wamejitahidi kwa njia ya vitendo kuwafuata wenzao na nyakati zingine kutosimamisha wagombea ili kupisha wanachama wa vyama vingine kugombea lakini bado wanakabiliwa na muitikio mdogo kutoka kwa wenzao.
Mfano:
Mwaka 1995 waliachia NCCR-Mageuzi kwenye ngazi ya Urais
Mwaka 2000 waliachia CUF kwenye ngazi ya Urais
Mwaka 2005 waliweka mgombea wa Urais na kuambulia nafasi ya 3
Kufuatia matukio hapo ilikubalika kuwa Mrema aachiwe nafasi ya Urais,lakini jimbo la Arusha aachiwe Mzee Mtei.Ilipofika wakati wa utekelezaji Makangoro Nyerere akasimamishwa na NCCR-Mageuzi na kunyakua ubunge wa Arusha mjini.Mwaka 2000 akaungwa mkono Prof.Lipumba kwa makubaliano yanayofanana na hayo ila bahati mbaya silikumbuki jimbo nao wakageuka na kusimamisha mgombea wa ubunge kinyume walivyo kubaliana na utaratibu wa kuachiana majimbo.
Hivi karibuni walianzisha tena ushirikiano wa vyama baada ya uchaguzi wa 2005.Ni bahati mbaya sana Mh.Wangwe akafariki dunia kipindi alichokuwa amesimamishwa uongozi ndani ya chama chake.Viongozi umoja wa upinzani wakashirikishwa na CHADEMA katika mazishi,ghilba iliyozushwa na CCM wakaingia mkenge na kukubaliana uzushi huo kuwa Mbowe na Mengi wamehusika kumua Wangwe.
Uzushi huo uliwahudhunisha sana wanachama wa CHADEMA nikiwemo na mimi mwenyewe kuona viongozi tulio na ushirikiano nao wanakubaliana na uzushi huo na kushabikia.Sisi wanacham tukashauri uongozi kwamab wenzetu hawatutaki wacha tujitegemee.Bada ya ushindi wa TARIME,ikatangazwa operesheni SANGARA ikiwa na lengo ya kutafuta kushikamana na wananchi tuachane na viongozi na muelekeo ni mzuri.
Ndugu yangu Mkandara harakati za kisiasa Tanzania zinapita katika kipindi kigumu,MAFISADI wa Tanzania wana nguvu kubwa hawawezi kuruhusu umoja wowote wa maana.Hata malumbano yanayoendelea sasa ya KIDINI yana mkono wao!
Huo umoja unapigiwa upatu na TISS(Disinformation Unit) naomba nyie wenye mapenzi mema na mageuzi tuunde a grand civil society(Tanzania Electoral Support Network) ikiwa supported na Radio yenye kusikika kwenye short wave ili kuwafikia watanzania walio wengi kwa wakati mmoja.Njia hiyo ilifanikiwa kumtikisa Dictator Mugabe kwa kutumia Zimbabwe Indipendence Voice(SW radioafrica).
Kutokana na hayo machache naomba kuto hoja!
 

Naam, umesema yote Mhe. Mkandara. CHADEMA bado wana kazi kubwa ya kufanya. Wanachohitaji ni kupata kura nyingi zaidi hata mara dufu ya zile za CCM ili hata uibaji wenyewe ushindikane!

Cha kusikitisha ni kwamba hakuna dalili yoyote ya vyama muhimu kuweza kuungana. Hivi sasa CUF wameanza kampeni za Chama chao na kwa maana hiyo ni kwamba hata uchaguzi utakapofika itabidi vyama vya upinzani wagawane kura za upinzani, jambo ambalo litazidi kuzorotesha 'ushindi' dhidi ya CCM.

Lingine ninaloliona kama setback ni kuibuka kwa viongozi wa dini kuanza kuonyesha dhamira na hisia zao kuhusu uchaguzi ujao. Hilo nalo ni hatari kwa sababu litawagawa wananchi kwa misingi ya dini. Ikumbukwe kwamba chama cha CUF kimekuwa kikihusishwa na dini ya Kiislamu kwa maana hiyo wananchi wasio na elimu ama mwamko wa kutosha wa kisiasa wanaweza kupotoshwa na kukiunga mkono chama cha CUF ama wale ambao si waislamu kutokiunga mkono kwa sababu ya dhana hiyo ya udini.

Chama cha Mapinduzi kifike hali kielewe kwamba kimekwisha kengeuka; Viongozi wa CCM wamekuwa walaghai, uadilifu hawana kiasi cha kuwafanya wananchi walio wengi na hata wana CCM wenyewe kutokuwa tena imani na chama hicho. Kinachofanyika sasa hivi ndani ya CCM ni uhuni na ubabe ambao utaweza kuleta madhara makubwa kwa mustakabali wa Taifa letu. Tuombe Mungu atunusuru na balaa lililombele yetu. Nakumbuka hadithi ya vyura na watoto waliokuwa wakirusha mawe mtoni. Vyura walilalamika kwamba mchezo wa watoto hao ni mauti kwao. Hakika, madhara yatakayotokana na mchezo mchafu wa CCM itakuwa mauti kwa Taifa!
 

Mkuu
ukiyangalia kwa ndani na mapana yake maandiko yako utagunduwa moja tu. Kwamba sisi Watanzania ndio tuna matatizo wala hakuna chama chenye matatizo ni sisi wenyewe, tunahitajika kubadilika.
 

Mimi nafikiri ccm wanafanya hivyo wakiamini kitu kimoja hata vurungu zikitokea ni kati ya wanachama wa chama husika na polisi/jeshi na si wananchi kwa wananchi ,umeipata point yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…