Invincible,
Mkuu nadhani umetuelewa vibaya. Mimi binafsi nawapongeza sanasana Chadmea kwa kazi kubwa waliyoifanya iwe majimbo yote ya Uchaguzi ambayo wameshikiri. Lakini hii sii dhamira ya mtazamo wangu wala mategemeo ya wananchi wengi. Tunachokitazama ni zaidfi ya hatua waliyofikia na kama kuna kwenda mbele zaidi ikiwa CCM wapo.
Mkuu CCM walishindwa na TLP wala sii muda mrefu ulopita na waliiba kura vile vile, leo hii Chadema wameingia na kuchukua kura zote za TLP lakini wameshindwa kuvuta toka CCM ndio maana CCM kaibuka mshindi iwe kaiba au hakuiba.. haya ya kuiba kura CCM hufanya chaguzi karibu zote na unatakiwa kumshinda kwa hesabu kubwa sana..Hivyo Chadema kimeweza kupiga hatua dhidi ya TLP na sii CCM (ambao wameibuka washindi) hii ndiyo reality nayojaribu kui explore..
Hivyo hivyo chaguzi za sehemu zingi zilizopita, utaona kwamba vita huanza na vita baina ya Upinzani, kisha wakagawanyika, CCM hingia kwa mlango wa nyuma wakaibuka washindi. Hii vita baina ya wapinzani ndio chanzo cha kushindwa. Wananchi hatutaki kuingia fainali wala kushiriki kwa vyama vya Upinzani tunachotaka sasa hivi ni kuonma suhindi unakuja upande huu. Hizi ahadi za Kikwete kutuhakikishia kwamba Tanzania itaingia World Cup mwaka 2010 wakati sisi wananchi hatuoni uwezo huo kuwepo ni mawazo ya kujenga tunapojadili na kuzungumzia mapungufu ya mchezo huo nchini...kamleta kocha wa nje na kadhalika hadithi ikasimama pale pale..Tanzania hakutufika hata fainali za nchi za Kiafrika..lakiuni muulize Kikwete na mawaziri wake kama alitegemea hali hii kutokea.. watakupa sababu mia kidogo na hawatakubali kwamba walifanya wao makosa hapa na pale..
Ndicho nachozungumzia mkuu wangu Waungane vichwa, chama au vyovyote vile vyama hivi vinatakiwa kusimamama pamoja (mshikamano) wakati wa uchaguzi na kuwa kitu kimoja against chama tawala..Laa sivyo CCM kila siku itaibuka mshindi kwa sababu CCM ina washabiki haina wapenzi wa nchi hii. Ndio maana tuna vazi la chama (njano na Kijani), hatuna vazi la taifa..Taifa bila CCM ni taifa lililopotea hii ndio imani ya dini inayotangazwa na huwezi kuwabadilisha kirahisi..
Mkuu Mkandara,
Nashukuru sana kwa ushauri wako,humu ndani ya JF ni miongoni mwa watu nikiona mabandiko yao huwa sisiti kuyasoma ya wengine nayaruka.Hilo pendekezo lako ni zuri sana na Wanachadema na wapenda demokrasia wote wanalikubali.
Ugumu upo kwenye utekelezaji viongozi wa CHADEMA kwa upande wao wamejitahidi kwa njia ya vitendo kuwafuata wenzao na nyakati zingine kutosimamisha wagombea ili kupisha wanachama wa vyama vingine kugombea lakini bado wanakabiliwa na muitikio mdogo kutoka kwa wenzao.
Mfano:
Mwaka 1995 waliachia NCCR-Mageuzi kwenye ngazi ya Urais
Mwaka 2000 waliachia CUF kwenye ngazi ya Urais
Mwaka 2005 waliweka mgombea wa Urais na kuambulia nafasi ya 3
Kufuatia matukio hapo ilikubalika kuwa Mrema aachiwe nafasi ya Urais,lakini jimbo la Arusha aachiwe Mzee Mtei.Ilipofika wakati wa utekelezaji Makangoro Nyerere akasimamishwa na NCCR-Mageuzi na kunyakua ubunge wa Arusha mjini.Mwaka 2000 akaungwa mkono Prof.Lipumba kwa makubaliano yanayofanana na hayo ila bahati mbaya silikumbuki jimbo nao wakageuka na kusimamisha mgombea wa ubunge kinyume walivyo kubaliana na utaratibu wa kuachiana majimbo.
Hivi karibuni walianzisha tena ushirikiano wa vyama baada ya uchaguzi wa 2005.Ni bahati mbaya sana Mh.Wangwe akafariki dunia kipindi alichokuwa amesimamishwa uongozi ndani ya chama chake.Viongozi umoja wa upinzani wakashirikishwa na CHADEMA katika mazishi,ghilba iliyozushwa na CCM wakaingia mkenge na kukubaliana uzushi huo kuwa Mbowe na Mengi wamehusika kumua Wangwe.
Uzushi huo uliwahudhunisha sana wanachama wa CHADEMA nikiwemo na mimi mwenyewe kuona viongozi tulio na ushirikiano nao wanakubaliana na uzushi huo na kushabikia.Sisi wanacham tukashauri uongozi kwamab wenzetu hawatutaki wacha tujitegemee.Bada ya ushindi wa TARIME,ikatangazwa operesheni SANGARA ikiwa na lengo ya kutafuta kushikamana na wananchi tuachane na viongozi na muelekeo ni mzuri.
Ndugu yangu Mkandara harakati za kisiasa Tanzania zinapita katika kipindi kigumu,MAFISADI wa Tanzania wana nguvu kubwa hawawezi kuruhusu umoja wowote wa maana.Hata malumbano yanayoendelea sasa ya KIDINI yana mkono wao!
Huo umoja unapigiwa upatu na TISS(Disinformation Unit) naomba nyie wenye mapenzi mema na mageuzi tuunde a grand civil society
(Tanzania Electoral Support Network) ikiwa supported na Radio yenye kusikika kwenye short wave ili kuwafikia watanzania walio wengi kwa wakati mmoja.Njia hiyo ilifanikiwa kumtikisa Dictator Mugabe kwa kutumia Zimbabwe Indipendence Voice(SW radioafrica).
Kutokana na hayo machache naomba kuto hoja!