CHADEMA: Baada ya Biharamulo; Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010

CHADEMA: Baada ya Biharamulo; Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Kwanza haina sababu ya kufanya hivyo. Pili, inachosha kusikia wimbo wao wa malalamishi kuhusu CCM, dola n.k lakini kubwa ni kupoteza mtaji wao wa kisiasa. Wamuunge mkono mgombea wa chama kingine wao fedha na raslimali ambayo wangeitumia huko kwanza warudi Busanda, Kiteto, Mbeya Vijijini, Tunduru n.k na majimbo mengine kama 70 tu na huko wajijenge kwa ajili ya 2010.

a. Kuandikisha wanachama wapya (kupata kura 22,000 si mchezo kwani kuna wanachama wangapi?)
b. Kufungua matawi mapya
c. Kutengeneza mtandao wa mafunzo kwa makada wake
d. Kutengeneza ajenda za mahali (hili nitalichambua baadaye)
e. Kubadilisha Katiba yake ili kilenge kushinda uchaguzi na kuunda serikali.
f. kulenga majimbo ya mjini ambako imekuwa ikikubalika kwa kufanya hayo ya a, b na c
g. Kubadili mkakati wa mahubiri yake, kuhubiri ufisadi hakuleti ushindi bali kuhubiri ujumbe wa matumaini dhidi ya ufisadi kutaleta. Wao watafanya nini. Hapa hawana budi kuradicalize their message. "tutawatafuta wale wote waliohusika na wizi wa fedha umma, tutawawajibisha, na walioficha fedha nje tutahakikisha zinarudishwa ndani ya muda x).
h. Wahamishe makazi yao toka Dar na kuamia vijijini; Dar iwe pa kuja kuchaji tu.
i. x,y
 
Last edited by a moderator:
- Waende wasiende haiongezi wala kubadili anything, dawa ni ku-do away na vyama vyote vya siasa bongo tuanze upya!

Respect.

FMES!
 
- Waende wasiende haiongezi wala kubadili anything, dawa ni ku-do away na vyama vyote vya siasa bongo tuanze upya!

Respect.

FMES!

hilo haliwezekani. Implication yake ni kubwa mno na haikadiriki. Unless by "tuanze upya" ina maana tuitishe uchaguzi mkuu mwaka huu!!
 
Sounds like great idea that Chadema can not afford to give away!
 
- Waende wasiende haiongezi wala kubadili anything, dawa ni ku-do away na vyama vyote vya siasa bongo tuanze upya!

Respect.

FMES!

Respect Mkuu FEMS, naona hapo umekuwa na munkari kidogo! Hebu tueleza sababu za kauli hiyo maana inaonyesha kujua mengi na kukata tamaa pia
 
Nakubaliana na Mzee Mwanakijiji 70%.
Nyongeza yangu ya 30% ni kwamba badala yake wamwezeshe Finias Magessa kwenda kortini ili akishirikiana na Mwanasheria wao maarufu Tundu Lissu, uchafu na madhambi yote yaliyotendwa na CCM huko Busanda yawe publicly exposed.
Hata kama Serikali ya CCM ita-interfere huko mahakamani na kuchelewesha final judgement against their candidate, publicity ya hayo madhambi itakuwa ni sehemu ya civic education kwa Watanzania wote.
Papo hapo viongozi wa Chadema waendelee na mkakati wao maarufu wa "Operesheni Sangara" kama walivyoahidi kwamba watazunguka mikoa yote ya nchi. Wakiwa na resources zaidi wanaweza ku-treat Biharamulo kama sehemu ya "Operesheni Sangara".
 
Last edited:
Mwanakijiji,
You must be kidding, hebu tazama takwimu za 2005, linganisha na hii zaidi ya 40% waliyopata Busanda, utajua kwa nini wanatakiwa waende Biharamulo. Mbeya vijijini CUF walisema waachiwe kwakuwa 2005 walikuwa wa pili nyuma ya CCM, wakafanya mizengwe kumuengua mgombea wa CHADEMA, wakapata chini ya 20%. Busanda hadithi ikawa hiyo hiyo ya kuwa wa pili 2005, wamepata chini ya 5%. Sijui strength ya CHADEMA kifedha, lakini kutokwenda Biharamulo litakuwa ni kosa kubwa sana kwani hiyo 40+ % achievement ya Busanda si jambo la mzaha na sambamba na op sangara, itakuwa pia nafasi yao ya kuimarisha chama. CCM wanalijua hilo!
 
Wanachama wa CHADEMA wa Biharamulo wanaohitaji mgombea wao ashiriki uchaguzi, wana lengo kwamba apite ama awe mshindi, ni vyema wakashiriki kujitambua nafasi yao katika jamii ya wananchi wa Biharamulo ipoje, wasije ishia kulalamika baadae pengine kura ziliibwa, ama kulikuwa na hujuma' Tusisahau tunapotamka CHADEMA tunazungumzia Chama na ni kundi maslahi ya watu
 
Nakubaliana na Mzee Mwanakijiji 70%.
Nyongeza yangu ya 30% ni kwamba badala yake wamwezeshe Finias Magessa kwenda kortini ili akishirikiana na Mwanasheria wao maarufu Tundu Lissu, uchafu na madhambi yote yaliyotendwa na CCM huko Busanda yawe publicly exposed.
Hiyo asilimia kwa kwenda Mahakamani ni mwanzo wa kukifanya chama hicho kuanguka na kupoteza umaarufu kama CUF, NCCR na vinginevyo ambavyo vimeshindwa kujua mbinu mbalimbali za kupiga kampeni.
 
22000 voters sio mcheze. Pongezi chadema.Kwa ujumla chama kina kuwa vizuri. Nakubaliana na mwanakijiji chama kijipange kimkakati (strategic). Sio mbaya kuweka nguvu mijini ambako elimu ya uraia ni kubwa kwani hili litaiwezesha chadema kupata wabunge wengi. Kuna haja ya chama kujipanga ki-ajenda- pamoja na ufisadi mtatekeleza maboresho gani? vipi watanzania wataendesha uchumi wao? Vipi watoto wetu na vitukuu wetu watarithi tanzania salama yenye maziwa na asali. Vipi utawala wa kisheria utazingatiwa? vipi tanzania itakuwa kiongozi ktk siasa, uchumu, regional intergration ktk ulimwengu wa leo. Vipi kuhusu wafanya biashara wazalendo?. Mambo kama haya yakielezwa vizuri hakika yatainyanyua chadema. La mwisho epukeni migogoro ya ndani try to sort out yourselves incase of misunderstanding.
 
Nashauri wafanye tathmini ya haraka na kupanga upya mikakati ya kuingia Biharamulo.

Mkuu mwanakijiji
Kwa siasa za bongo ambazo zimegubikwa na jinamizi la sera za uongo za sisiemu, nadhani kwa kipindi hiki ni budi wapinzani wakatumia pia silaha ya lawama kwa chama tawala kushindwa kutekeleza ahadi zake since uhuru na wakati huo huo wakinadi sera zao zinazotekelezeka na si ahadi za kugawana posho za ubunge na wananchi.

Tathmini ifanyike mapema na wasimsake mchawi wao kwani bado elimu ya uraia haijaingia kisawasawa kwenye wananchi wengi wa Taifa hili tukuka. Nasisitiza hata vyombo vya dola vya sheria vinapaswa kuelimishwa kuhusu demokrasia na kutenganisha utawala na masuala ya ndani ya vyama. Inawezekana wananchi wakaelewa wajibu wao ila dola ikaendelea kutojitambua.
 
Respect Mkuu FEMS, naona hapo umekuwa na munkari kidogo! Hebu tueleza sababu za kauli hiyo maana inaonyesha kujua mengi na kukata tamaa pia

- Mkuu wangu unajua kina Nchimbi wapo wanasubiri pembeni kuchukua power, hivi kweli unategemea mabadiliko karibuni? Kuna wengine tumechoshwa na hii political drama ya bongo! Tuna miaka 50 zaidi ya hii drama za kudanganyana tu progress hakuna, pande zote mbili zinatudanganya tu wananchi! wote waende tuanze upya!

Respect.

FMES!
 
Kwanza haina sababu ya kufanya hivyo. Pili, inachosha kusikia wimbo wao wa malalamishi kuhusu........

c. Kutengeneza mtandao wa mafunzo kwa makada wake


Mwanakijiji leo umenikosha sana hope waliopo hapa watawafikishia unabii huu wenzao.
Red: bora umesema wewe kiazi niliposema mimi mhogo niliambiwa na mzizi
blue: Hii ndio njia ya ukombozi; hata wale wafuasi wa Marx wana amini ukombozi wa fikra ndio injini ya mapinduzi ya kweli. Tutumie pesa za mafuta ya helkopta na posho za akina mwita kufanya mafunzo kwa makada wa vyama vyetu ikibidi hata tuanzishe na sisi magogoni yetu haraka.
 
kupoteza mtaji wao wa kisiasa. .

this is WRONG!mtaji wao KISIASA ni pamoja na kupanua wigo wao kwa kupata wanachama wengi.kugombea kutawasaidia kuwapata wanachama wengi pia kuamsha fikra za watanzania wengi juu ya kinachoendelea ndani ya chama na serikali tawala.kupata wanachama wengi ni a LONG TERM STRATEGY,na kushinda uchaguzi wa busanda 'it was another cup of tea'.
kwa chadema mimi nawashauri waichukue kama challange.







a. Kuandikisha wanachama wapya (kupata kura 22,000 si mchezo kwani kuna wanachama wangapi?)
b. Kufungua matawi mapya
c. Kutengeneza mtandao wa mafunzo kwa makada wake
d. Kutengeneza ajenda za mahali (hili nitalichambua baadaye)
e. Kubadilisha Katiba yake ili kilenge kushinda uchaguzi na kuunda serikali.
f. kulenga majimbo ya mjini ambako imekuwa ikikubalika kwa kufanya hayo ya a, b na c
g. Kubadili mkakati wa mahubiri yake, kuhubiri ufisadi hakuleti ushindi bali kuhubiri ujumbe wa matumaini dhidi ya ufisadi kutaleta. Wao watafanya nini. Hapa hawana budi kuradicalize their message. "tutawatafuta wale wote waliohusika na wizi wa fedha umma, tutawawajibisha, na walioficha fedha nje tutahakikisha zinarudishwa ndani ya muda x).
h. Wahamishe makazi yao toka Dar na kuamia vijijini; Dar iwe pa kuja kuchaji tu.
i. x,y

hapa sawa....!
ni strategies nzuri sana hizi.tena wakigombea biharamulo wataongeza maeneo ya kufanya implementation ya hizo points tajwa hapo juu
 
Ishiriki!!

Pia waendelee kudai Independent National Election Commission

Haya mambo ya DED kuwa mkuu wa uchaguzi wa wilaya na Raisi kuteua Tume ya uchaguzi vyama vya upinzani vitabaki kulia wameibiwa miaka zaidi ya 50 ijayo upo upendeleo wa wazi kwa sisiemu

We need to change Constitution otherwise ni kilio kila siku za uchaguzi
 
Jamani ukweli ni kwamba ccm haiwezi kushindwa as long as katiba iliyopo haijarekebishwa!! Karibu uchaguzi wa mitaa unakaribia, na mpaka sasa sio swala la katiba tu bali hata lile la INDEPENDENT candidates bado halijapatiwa ufumbuzi unaotekelezeka.Vyama vya upinzani kama kweli hawawanii RUZUKU tu basi ni vyema wakayafanyia kazi mambo hayo mawili kwanza halafu mengine yatafuata.
 
Ishiriki!!

Pia waendelee kudai Independent National Election Commission


waendelee kudai kwa nani? for how long?

hili linawezekana tu,IWAPO KATIBA ITABADILISHWA.sasa utata unakujaje,katiba ipo IN FAVOUR of the existing power!(ndo watu ambao wapinzani wanashauriwa WAENDELEE KUWADAI)

katiba itabadilishwaje?......................


Raisi kuteua Tume ya uchaguzi vyama vya upinzani vitabaki kulia wameibiwa miaka zaidi ya 50 ijayo upo upendeleo wa wazi kwa sisiemu

madaraka ya rais yamekuwa mengi kupindukia!tatizo ni huu msahafu(katiba)
katiba itabadilishwaje?......................wakati inawafeva wao


We need to change Constitution otherwise ni kilio kila siku za uchaguzi

Naomba kurudia swali,KATIBA ITABADILISHWAJE?.........
 
Mimi naunga mkono wazo la Mwanakijiji,kushiriki katika mazingira haya tuliyonayo ni vigumu mno.Wanamageuzi washawishi vikundi vya kijamii kama vile FEMACT,Baraza la Maaskofu(TEC) na asasi zingine za kijamii kudai mabadiliko ya katiba.Dalili zimeshaanza kujitokeza kwa Asasi nyingi sasa hivi zimeshaanza kuthubutu kuhoji mwenendo wa serikali dhidi ya mafisadi na miradi ya kifisadi iliyoibuliwa hivi karibuni na wanaharakati mbalimbali.
Tutumie hii momentum kushinikiza a grand coaliation kama ile ya Zimbabwe(Zimbambwe Electoral Support Network) kwa asasi zetu za kijamii.Tusiiache CHADEMA ifanye kazi hiyo,mabadiliko yeyote tunayoyatafuta yatapatikana tu ikiwa kila mmoja wetu atakuwa chachu ya mabadiliko.Hoja ya FMES haiwezi kusaidia kuleta mageuzi haya tukiachia vyama vya siasa kuletea mabaduliko tunayo yataka.Naomba sana wanaharakati popote pale mlipo muache kushabikia vyama siasa kipindi hiki tujikite kutafuta katiba mpya ambayo itazingatia hali tuliyonayo sasa hivi.
Angalizo mojawapo ni mamlaka makubwa ambayo tumembebesha Rais as if nchi hii ni ya mtu mmoja.Haiwezekani kukawa na utawala unaofuata sheria,wakati mhimili mmoja umeelemewa na majukumu mengi ambayo yameshindikana kuleta ufanisi na ufumbuzi wa matatizo mbalimbali yanayorikabili Taifa.Wenzetu mlioko huko tutafutieni wanaharakati ili wasaidie kuanzisha Radio kama ile ya Zimbabwe Independence Voice(SW Radio Africa) ambayo itasikika kwenye short-wave.
Naamini kabisa tukitekeleza hayo,Elimu itawafikia wapiga kura na kuleta tija tunayoitamani sana!
 
Back
Top Bottom