Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
TAARIFA KWA UMMA
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa jana Novemba 08, 2024 akizungumza Waaandishi wa Habari jijini Dodoma alisema kuwa wagombea walioenguliwa wakate rufaa na kuwa rufaa hizo zitasikilizwa kwa haki.
Baada ya kauli hiyo ya Waziri jana, leo Novemba 09, 2024 tunapokea taarifa kuwa ofisi za watendaji wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji zimefungwa kuanzia Bukoba Vijijini, Dar es salaam, Simiyu, Solwa, Bariadi na maeneo mengine nchini.
Mosi, tunaitaka TAMISEMI ielekeze Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wawepo ofisini ili kupokea mapingamizi yetu.
Kupata habari za Uchaguzi Serikali za Mitaa kimkoa bofya hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Pili, TAMISEMI ifungue mlango mwingine wa kupokea mapingamizi ikiwa watendaji wataendelea kukaidi amri ya kuwa ofisini. Hii ikifanyika itatuthibitishia kuwa kufunga ofisi ni maelekezo ya TAMISEMI kwa watendaji hao.
Tatu, tunataka kuona hatua za kinidhamu zikichukuliwa dhidi ya Watendaji na Wasimamizi wote ambao wanaharibu Uchaguzi Kwa makusudi huku wakijua kufanya hivyo kunaweza kulitumbukiza Taifa kwenye machafuko.
Nne, kuna Wasimamizi wa Uchaguzi ambao wameondolewa kwenye nafasi zao baada ya kufanya uteuzi jana, kama Buhigwe, Kigoma wameshushwa vyeo na kuteuliwa wasimamizi wapya.
Tunataka kujua sababu za kuondolewa kwao, kwani huu ni uthibitisho kuwa TAMISEMI inaelekeza hivyo. Tunawataka Wanachama, Wagombea na Viongozi wetu wa maeneo yote walioenguliwa, wakate rufaa na kwenda kuziwasilisha kwenye ofisi za watendaji na kama zimefungwa ofisi hizo wakae hapo mpaka ofisi zitakapofunguliwa na watendaji kupokea mapingamizi yetu.
Imetolewa leo Jumamosi tarehe 09 Novemba, 2024
John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya nje.