Chadema badala ya kupigania Tume huru ya uchaguzi wao wanataka NEC isimamie uchaguzi wa Serikali za Mitaa badala ya TAMISEMI

Chadema badala ya kupigania Tume huru ya uchaguzi wao wanataka NEC isimamie uchaguzi wa Serikali za Mitaa badala ya TAMISEMI

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kuna wakati ukivifikiria hivi vyama vya upinzani unaelewa ni kwanini CCM inaweza kuongoza hii nchi kwa namna inavyotaka.

KUB anaomba eti NEC ndio isimamie uchaguzi wa serikali za mitaa badala ya waziri wa Tamisemi.......yaani anaamini hapo ndio haki itatendeka.

Binafsi sioni tofauti kati ya NEC na Jaffo kwa sababu hata uchaguzi mkuu wasimamizi ni wakurugenzi ambao wako chini ya waziri wa Tamisemi.

Kiukweli hapa tulipofika hatuna upinzani nchi hii bali tunao mfano tu wa upinzani.

Yaani badala ya kupigania Tume huru ya uchaguzi wewe unapendekeza tume inayoteuliwa na mwenyekiti wa CCM iongezewe majukumu?

Upinzani ni bure kabisa.......ruzuku yetu ni bora wapewe wanafunzi wa elimu ya juu itasaidia taifa siku za usoni.

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom