Uchaguzi 2020 CHADEMA bado tishio kubwa Uchaguzi Mkuu

Uchaguzi 2020 CHADEMA bado tishio kubwa Uchaguzi Mkuu

Kila msema kweli ataambiwa ni CDM hiyo,mpinzani,wakala wa beberu(Kuwadi?),mchochezi na majina kama hayo.Watetea maovu tuwaite CCM?

Watanzania turudi kwenye ile misingi yetu ya asili ya Amani na upendo,tuepuke chuki,ubaguzi,unyanyasaji,uvunjifu wa sheria na katiba.Mlinzi wa nchi yetu ni Sisi sote na tusiruhusu wanaovunja katiba.

Kama kuna chama Tawala bora hapa kwetu waruhusu shughuli za kisiasa kwa usawa na tuache Wananchi wachague viongozi wao bila figisu tuone nani wanapendwa kuwawakilisha.
Ukitaka hayo uliyoyasema, omba serekali ya chama kimoja tuu, sio vyama vingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli bado Ni mchungu, Chadema bado tishio uchaguzi mkuu. Kuna dalili kuu nyingi kwamba CCM wanaingiwa hofu kwa jina la Chadema.

Viongozi wa Chadema hawaruhusiwi kuongea na wakiongea utawasikia polisi wakiwaita au kukataliwa kabisa kuongea. Hii Ni hofu kubwa kwa CCM na serikali yake. Ukifuatilia mienendo na hukumu za vyesi vyao bado utagundua Ni kutokana na hofu ya kuwapora madaraka CCM.

Sehemu nyingine Ni kampeni ya mapema ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu. CCM imetumia vyama jukwaa la siasa takribani miaka yote 5 hii kujinadi kutoa ahadi kupitia kwa mwenyekiti wao.

Pia mazingira ya hamahama kwa wabunge wa upinzani na figisu kufanyika kuwarudisha wabunge walewale kwa kuminya uchaguzi kuwatangaza kwa lazima Ni dalili tosha kuwa CCM haiwawezi Chadema kwenye chaguzi huru.

Polisi na wakurugenzi ambao pia Ni makada ya chama wamehakikisha wanavuruga chaguzi za marudio ili kuwapa CCM ushindi.

Mahala pengine wakuu wa usslama polisi wsmesikika wskijinadi kuwa chama pekee Ni CCM bila kuchukuliwa hatua. Hii Ni pamoja na kuwabambikia wafuasi wa Chadema vyesi na kuwaweka ndani na kuwanyima dhamana.

Mambo Ni mengi Ila kipenga kitakapopulizwa na uwanja kuwa bila miiba Basi CCM inaweza kuondoka. Kikubwa Ni utulivu na haki itendeke.

Nakubaliana nawe TULIONA KATIKA UCHAGUZI WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA.
 
Back
Top Bottom