Ni wazi kuwa kupata katiba mpya hakuwezi kuwa kwa lelemama.
Ni wazi kuwa uwepo wa wahafidhina wenye maslahi na katiba iliyopo ndiyo kilicho kikwazo pekee.
Ni wazi kuwa wenye uthubutu wa kuzisukuma mbele jitihada hizi takatifu za kuwafanya wahafidhina hawa kusikia ni Chadema.
Ni wazi kuwa kwenye hili wingi wetu na utayari wetu wa kuyajaza magereza yao ndiyo iliyo karata ya turufu.
Hata hivyo Chadema nao wanatuangusha kwenye haya:
1. Kukosekana kwa uongozi usiotetereka (muda wote) wa kuyasukuma mbele (spearhead) madai haya halali ya wananchi ya kudai katiba mpya.
2. Kukosekana kwa mkakati wa wazi usiotatizika wa kudai katiba mpya.
3. Kukosekana kwa mkakati wa wazi wa kuwahami wahanga wote ambao ni lazima watakuwapo kwenye harakati hizi.
4. Kukosekana kwa mkakati wa wazi wa kuwahusisha wote watakao kuchangia harakati hizi, usiomnufaisha mtu yeyote kama fursa.
5. Kukosekana kwa mkakati wa wazi wa kuyajaza magereza yao pomoni.
Wananchi tuko tayari.
Kule juu palihitaji wapambanaji wasiochoka wa aina za kina Mandela, Oliver Tambo, Cyril Ramaphosa, Chris Hani, Solomon Mahlangu, Steve Biko na wa namna hiyo wa enzi za ukombozi.
Hapa kwetu uongozi wa washupavu kama akina Aboubakar Mbowe, Lema, Heche, Lissu, na wa namna hiyo ambao hofu kwao mwiko na kuaminika kwao ni kama wote ni lazima uwepo muda wote.
Damu haipaswi kulala!
Huu si muda wa kuangaliana usoni na kuoneana haya. Huu ni muda wa kuangaliana usoni na kupeana makavu kwa mustakabala mwema wa mapambano haya.
Wenye hofu na wakae pembeni kiroho safi tu. Wasiokuwa na ujasiri unaotakikana watupishe.
Wavumao baharini papa, lakini na wengine wapo!
Magereza yakijaa kesho hata Mh. Mbowe anatoka kesho hiyo hiyo wala kesi hamna.