Dah!!
Ndugu yangu kama umesoma,jaribu kuonesha kama Elimu imekukomboa.
Vinginevyo utaonekana kua umeikomboa Elimu.
Siku nchi hii itapata katiba mpya,ni siku wananchi wataitaka katiba hiyo.
Kwasasa ni ngumu. Jaribu kuelewa.
Mnauliza kwani CHADEMA siyo wananchi?
Nikiri,ni wananchi. Ila kwasasa,CDM kudai katiba inaonekana kama kikundi cha watu,tena wahuni tu,kikundi kisicho na adabu kwa serikali iliyopo.
Yamefanyika majaribio kibwena ya kudai katiba mpya,au kubadilisha baadhi ya mambo ndani ya katiba,hakuna lililofanikiwa isipokua walilotaka CCM wenyewe.
Ndiyo maana nakuambia,bado mno kuipata katiba mpya.
Mmesahau UKUTA,M4C,SANGARA,na nyingine nyingi zilivyozima bila mafanikio yoyote?
Nchi hii ni ngumu mno kuwafanya watu wake waelewe unachotaka waelewe.
Pia,nchi hii imeishi kwa mifano ya majirani au yanayotokea duniani.
Kenya hapo,walipata katiba mpya,kiko wapi?
Matatizo yao yaliisha?
SA tunaambiwa wana katiba bora,matatizo yao yameisha?
Mifano hii ndiyo inawafanya Watanzania kuishia kuiamini CCM na kuichagua kila mwaka achilia mbali kelele zenu kuwa huwa mnaibiwa kura,japo ukweli huwa mnabaki nao mioyoni mwenu.
Narudia tena,toeni Elimu kwanza,Elimu ikikolea,haya mnayoyaforce yatokee leo,yatatokea kirahisi mno.
Sent using
Jamii Forums mobile app