Kuishinda CCM ni Maji kwa Bilauli...
Chadema wanatakiwa kufanya yafuatayo...
1. Waweke powerful powepoint presentation (fupi si chini ya dk 2) ya nini wanafikiri ni matatizo ya nchi yetu, na watoe katika presentation hiyo ni nini wanataka kukifanya ndani ya miaka mitano ambacho ccm wameshindwa kukifanya zaidi ya miaka 40, waache kuwa-criticise CCM na waseme tu ccm imejenga nyumba inayohitajika kuimarishwa na mafundi wengine kwani wao kila walipojenga , nyumba humomonyoka kila kukija masika na inafaa kubadili fundi ili nyumba itengemae wakati wote ije masika kije kiangazi...
2. Chadema wajue Tanzania ina idadi ya vijiji vingapi, wagawe siku za kampeni na wavifikie robo tatu ya vijiji vyote vya tanzania na suluhisho la matatizo yetu bila kuwa-ctiticise ccm, wawape moyo matumaini watanzania wapiga kura na kusema kwamba tanzania ya neema inawezekana bila ya ccm.
3. Waweke kitengo maalum ya utafiti na wanasheria ili kuwashitaki ccm haraka iwezekanavyo mara inapothibitika kwamba ccm either wametoa takwimu za uongo, au za kukipaka matope chadema... pia kitengo hiki kifanye utafiti na kuwawekea pingazi wana ccm wagombea ubunge wote wenye mushkeri kisheria au kimasomo.
4. watafute lugha rahisi kabisa ya kuongea na mpiga kura , itayoeleweka bila utatanisho na cha msingi hapa ni kuhakikisha kwamba wapiga kura wanaelewa ni nini chadema inawaambia, na wanakielewa, wanakitafakari na kukiamini wanachoambiwa , na wanawashia moyo wa matumaini ya kwamba uchaguzi uje haraka ili chadema kichaguliwe...
5. Waweke slogan fupi watakayo hakikisha kwamba kila mtu , hata mtoto anaijua kwa mfano... MAFISADI WANAPETA, WALALAHOI WANAPETESHWA MAGEREZANI... chagua chadema ikuondolee matatizo yako ya msingi... (Afya, miundombinu, elimi ya bure kwa kira mtu toka chekechea hadi chuo kikuu, umeme usiokatika siku 365 za mwaka na mengine mengi)
Ni hayo kwa sasa.. nitaongeza mangine baadae