Elections 2010 CHADEMA Campaign Machinery

Asante E the T ni kweli nguvu ya chama ni vijana. Chadema isilale time is not on our side. CCM wana uwezo wa kipesa kampeni yao inaongozwa na nguvu ya pesa na ukubwa wa chama lakini si scientific campaign.

Najua Chadema uwezo wakipesa si mkubwa lakini wakitumia the little resources walizonazo kwa makini inaweza ikazaa matunda mengi zaidi ya CCM. Kampeni za CCM ni sawa na shamba kubwa bila mbolea mazao yake yanaweza kulingana na shamba dogo lenye mbolea.

Kama Chadema wakiigawa nchi kikanda za uchanguzi inaweza kusaidia kuliko ku centralize kampeni. Kwa mfano kuwe na kanda sita kama nilivyoshauri, kila kanda wachaguliwe vijana kama 100 au 200 wapewe mafunzo ya kukampeni nyumba kwa nyumba hii inafanyika hata katika nchi zilizoendelea Obama alifanya na Cameron pia alifanya.

Kama alivyosema E the T hao vijana wapewe nyezo kama vipeperushi baiskeli nk ikiwezekana hata posho ya siku. Kuwe na center ya kampeni kwa kila kanda, kama Chadema hakina ofisi sehemu hizo ikiwezekana kigharamie kukodi vyumba au hata nyumba kwa kipindi cha miezi minne hadi sita , na hicho kiwe kituo cha kupatia informations zote za kanda hiyo to and from the Headquarters Office HQ.

Ninacholenga ni effective and scientific campaign, mawasiliano yawe ya hali ya juu na ya haraka, wasitegemee sana mawasiliano ya simu, effective communication is physical contact. Kama Chadema watakuwa na uwezo wa kupata helicopta mbili au tatu, wakati zingine zikiwa kwenye presidential campaign team helikopta moja iwe ya kitengo cha communications kazi yake ni kukusanya informations tu kutoka sehemu mbalimbali hasa kwenye vituo vya kanda za uchaguzi. Hii inawezekana.
 

Shukrani Sabi Sanda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…