CHADEMA dira yenu ya Chama ni ipi?

CHADEMA dira yenu ya Chama ni ipi?

Wanaukumbi.

Ngorongoro, Burj Khalifa, Ukraine, Katiba, Zitto, Mwenyekiti, Jiunge Mnyororoni, Zelenskyy Kidume, kuichukua Zanzibar, Dokta Slaa, Royo Tua, Bunge La Space kila wiki, mbona kama mambo ni mengi sana mtaweza kweli kwenda nayo yote kwa pamoja pamoja na Katiba mpya huku kila mmoja kajifungia chumbani kwake anachangia bunge la Space wengine Canada wengine Tarime.

Bongo za wanacdm zina processor kubwa hivyo zinaweza kuchakata mambo mengi kwa mpigo bila tatizo. Ila bongo za wanaccm processor zake ni Pentium one ndio maana zinaweza kuchakata wizi wa kura tu.
 
Wanaukumbi.

Ngorongoro, Burj Khalifa, Ukraine, Katiba, Zitto, Mwenyekiti, Jiunge Mnyororoni, Zelenskyy Kidume, kuichukua Zanzibar, Dokta Slaa, Royo Tua, Bunge La Space kila wiki, mbona kama mambo ni mengi sana mtaweza kweli kwenda nayo yote kwa pamoja pamoja na Katiba mpya huku kila mmoja kajifungia chumbani kwake anachangia bunge la Space wengine Canada wengine Tarime.

Tatizo lako mawazo kinzania unasema CHADEMA. Msimamo wa Chadema unatolewa na kiongozi wa chama kwa taarifa rasmi sio mitandaoni. Shida yako maoni ya wananchi yasiyokufurahisha unadai Ni ya CHADEMA.

Baki kwenye serikali ya CCM yenye dira ya kukopa na kulima tozo mbalimbali. Kwasasa Ni fahari kukopa kwa wazungu. Na World Bank imeionya Tanzania kuhusu kukua kwa Deni.
 
Mleta mada nilidhani una lengo la kuleta mada ya kujadili lakini ulichokiandika ni kejeli dhidi ya CHADEMA kwa 100%. Yote kwa yote nitakusaidia kuelewa kwa kifupi sana dira ya CHADEMA hapa hapa JF.

Dira kuu ya CHADEMA ni Demokrasia (kupigania uhuru wa kila mtanzania katika kuamua hatma ya maisha yake ya kila siku ya kisiasa, kiuchumi na kijamii) na Maendeleo (kupigania maendeleo ya mtu mmoja mmoja na jamii nzima pasipo vikwazo au kubaguliwa)

Sasa usishangae kwa nini CHADEMA wako busy kuhoji au kukosoa chochote kinachoendelea hapa Tanzania kwa kuwa dira yao ya kupigania Demokrasia ina akisi msukumo wa namna hiyo.
 
Wee mzee wewe. Sera ya Chadema ni kuto-omba omba. Mbona mnampenda kuomba omba sana. Mna nini nyie watu? Mtu anatoka nje kuomba mnampokea kwa ngoma kisa amepewa ''vifedha''! Haa haa haa! Kweli akili ni nywele na kila mtu ana zake. Nchi yetu imejaa utajiri lakini watu hamjiamini?
Wee jamaa una maanisha unachokisema au unawananga CDM kimtindo
Yaani CDM hawahawa wazee wa Jon za Chen au milion people challenge ??
Mbona wanachangishana bukubuku?
 
Wanaukumbi.

Ngorongoro, Burj Khalifa, Ukraine, Katiba, Zitto, Mwenyekiti, Jiunge Mnyororoni, Zelenskyy Kidume, kuichukua Zanzibar, Dokta Slaa, Royo Tua, Bunge La Space kila wiki, mbona kama mambo ni mengi sana mtaweza kweli kwenda nayo yote kwa pamoja pamoja na Katiba mpya huku kila mmoja kajifungia chumbani kwake anachangia bunge la Space wengine Canada wengine Tarime.
Mbona mnajichanganya? Baba yenu Mwendazake alisema ameiua Chadema sasa unaniuliza Dira gani?
 
CHADEMA ile kampeni ya “Join The Chain” matokeo yake ni nini?
Tunaona sasa kuna kampeni Mpya ya “One Million Challenge” bado kuna michango “GoFundMe”
Michango Michango Michango
Wananchi masikini wanatoa wapi hela kila siku kuwachangia Tu. Chama kinafanya siasa miaka 30.
 
Dira ya chadema ni "mbowe siyo gaidi na jiunge na mnyororo". Una swali la nyongeza?
 
Chadema kwenye dira walishapita kinachosubiriwa ni ccm kukubali kumalizia alipoishia warioba ili ccm iachane na ajenda za ukwapuaji wa uchaguzi ....
 
CHADEMA ILITUMIA MILIONI 377 NJE YA BAJETI

- Ukaguzi umebaini Tsh. 100,000,000 zilitumika kwa shughuli
ambazo hazikuwepo kwenye bajeti
- Chama kilinunua Magari 5 kwa 227,430,000 na kutumia

50,000,000 kununua nyumba ya Ofisi Kanda ya Serengeti.

Siyo mimi ripoti ya CAG
 
Back
Top Bottom