Chadema Kanda ya Kati wanazungumza muda huu mbele ya waandishi wa habari katika ofisi yao iliyopo Swaswa, Dodoma
"Sisi kama CHADEMA, Dodoma Mjini tuko imara kuliko siku zote. Hatuyumbishwi wala hatuna tamaa. Hatuhitaji kuwa na mihemko ya kisiasa. Tumechaguliwa na wanachama, tumeomba kuongoza chama hiki kukitoa pale kilipo na kuwatoa Watanzania walipo na kuwapeleka kwenye nchi ya amani na haki."
"Hatujaja kuomba uongozi huu kwa ajili ya tamaa za uongozi mwingine wa kiserikali, bali tumeomba uongozi huu kwa ajili ya kuikomboa Tanzania yetu."
"Nikiomba kuwa Mwenyekiti wa Wilaya au Mkoa, au Mwenyekiti wa Kanda, sihitaji fursa zaidi ya kuwakomboa Watanzania. Lengo la chama ni kushika dola. Lengo la chama si kupata ruzuku ya serikali."
"Kuna wengi mmekuwa mkiwasikia wakipiga kelele tu kwamba tumekosa maono. Mimi najiuliza, unakosaje maono wakati wewe ni Mwenyekiti wa Wilaya, Mwenyekiti wa Mkoa, Mwenyekiti wa Kanda, Katibu wa Kata, Mjumbe wa Mkutano Mkuu, Mjumbe wa Halmashauri Kuu au wa Baraza Kuu? Kwa sababu hizo ndizo ndoto tulizokuwa tukizihitaji – tuwe viongozi wa kwenda kulipigania Taifa na Watanzania, tupiganie haki ya Watanzania."
"Wanahama CHADEMA, si kwamba wanahama kwenda kutafuta fursa, bali wanahama kwa kutaka vyeo. Lakini nyie wenyewe waandishi wa habari mnaona – Watanzania wamekubali kutetea haki. Wanaoka pamoja, na ingawa kuna vitu vingi vinavyofanyika – unyanyasaji mwingi, kunyimwa viwanja vya mikutano – Watanzania wako tayari kufanya mikutano hiyo hata ufukweni kwa gharama zao, ili kuhakikisha kauli mbiu ya ‘No Reforms, No Election’ inapamba moto na kuendelea."
"Nia ya 'No Reforms' ni kuonyesha tunataka nini. Sisi hatuhitaji kutetea Watanzania tukiwa bungeni, wala madiwani. Tunahitaji Watanzania wapate haki yao."
"Bunge la Tanzania halina viti hata 400 lakini Watanzania tupo zaidi ya milioni 60. Sasa, ni Watanzania wote wanaokwenda Bungeni? Na kama kuwatetea Watanzania ingekuwa kwenda Bungeni au Halmashauri, basi kwenye Bunge la Katiba walikuwepo Wabunge wengi sana walioteuliwa — mliona… Katiba Mpya pendekezwa mpaka sasa haipo."
"Huko wanakokwenda wote hawaendi kuwa Wabunge wala Madiwani, bali wanaenda kunyanyasika na Chama cha Mapinduzi. Chama cha Mapinduzi kinatumia mkono huu mkubwa kutikisa watu kuwaambia wahamie chama kingine ili waonekane walifanya Uchaguzi Huru na Haki, kitu ambacho hakiwezi kutokea."
"Hivi ninavyoongea na nyinyi, Chama cha Mapinduzi washaiba uchaguzi. Wamejihakikishia kuiba uchaguzi kupitia kwenye kanuni zilizotungwa na Tume Huru ya Uchaguzi — inaitwa Tume Huru ya Uchaguzi."
"Kuna watu wanahama wanamsingizia Mbowe hata kama Mbowe yupo kimya, kwa sababu hivi hawa wote mnaowaona, Mbowe alikuwa anawasaidia nini? Kwanini wanabeba watu? Wakati wanaingia kwenye chama walikwenda kualika watu? Kwanini wakati unahama unaita waandishi wa habari wakati unaingia hukuita? Unaenda saluni, unajiandaa, unaita waandishi kwamba 'mimi leo ninaondoka CHADEMA'?"
Hongereni kwa msimamo thabiti
Pamoja tutaifikia nchi ya ahadi