CHADEMA Dodoma: Tumemchoka Mbowe, muda wake umeisha ampishe Lissu

CHADEMA Dodoma: Tumemchoka Mbowe, muda wake umeisha ampishe Lissu

Joined
Nov 19, 2024
Posts
94
Reaction score
307
Viongozi wa Majimbo 8 wa CHADEMA Mkoa wa Dodoma wamejitokeza hadharani kumuunga Mkono Mgombea wa Uwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu na kumtaka Mgombea mwenzake ambaye ndiye Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe kukubali kuwa wakati wake umepita hivyo ni wakati wa kukubali mabadiliko ndani ya chama hicho.

Akitangaza msimamo huo leo tarehe 19 Januari, 2025 kwa niaba ya wenzake Mwenyekiti wa Chama hicho Dodoma Mjini Stephen Karashan amesema iwapo Mbowe atashinda basi watafanya maamuzi magumu kwani wanajua maumivu waliyoyapata kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa katika kutafuta wagombea kwani wengi mioyo yao imekosa imani, hivyo mabadiliko yataongeza chachu ya watu kukipenda chama

Majimbo hayo ni Dodoma mjini, Kondoa vijijini, Chemba, Chamwino, Bahi, Kongwa, Kibakwe, Mpwapwa
 
Sindikiza na video kama wenzako Mkuu, tuwafahamu kwa sura hao mashujaa.

Lakini, haya yote wanayoyasema hadharani wahakikishe wanayafanya sirini kwenye kupiga kura nako pia wamuunge mkono Lissu.
 
Habari kama hii haiwapendezei kabisa ccm na chawa zake kwa sababu wana kikubwa sana cha kupoteza endapo Mbowe atapigwa chini.
 
Back
Top Bottom