Sir robby
JF-Expert Member
- Jun 22, 2022
- 2,396
- 4,080
Hakika nimefurahishwa sana jinsi Rais Samia anavyofanya siasa zake. Hakika huyu mama anaijua siasa sana kuliko mtangulizi wake, hayati Rais Magufuli.
Kitendo cha kukubali kufanya maridhiano na Chama Kikuu cha Upinzani CHADEMA, wakati hayati Rais Magufuli aliombwa na Mbowe lakini alikataa, kinampa ushindi mkubwa huyu mama kuwa anaijua siasa. Hongera sana Rais.
Kwa upande wa CHADEMA, najua mpo kwenye maridhiano na CCM kutokana na yote yaliyotokea katika utawala katili wa Awamu ya 5, utawala uliowatisha na kuwarubuni wanachama wenu Halima Mdee na wenzake 18.
Binafsi, naamini kwa asilimia 100 kuwa ubunge wao wa viti maalum ulipewa na mtawala wa Awamu ya 5 kwa vitisho vikubwa ili kuwahadaa wahisani kutokana na bunge kutokuwa na kambi ya upinzani na kuidhoofisha CHADEMA, na sio Halima Mdee na wenzake 18 waliutafuta huo ubunge.
CHADEMA mnamjua vizuri mtawala wa Awamu ya 5. Hebu jiulizeni yule mwanachama aliyekuwa gerezani aliwezaje kutoka jela tena usiku na kwenda kuapa, kama sio agizo la mtawala?
CHADEMA, fanyeni maridhiano na Halima Mdee na wenzake 18 ili warudi kundini.