CHADEMA haifai kabisa kuongoza nchi kwa sasa Tujipange haswa! Kuna Mkanganyiko

mbowe amepambana mno, kwa muda aliokaa madarakani, legacy yake inaheshimika.
kwa busara tu amalize muda wake aache new direction impokee uongozi wa chama, mbowe ameshaingia umri ambao hayuko tayari kwa kshkash yoyote, apumzke abak kwenye baraza la wazee.
msitegemee kumuona mbowe mpambanaji, muda aliokaa madarakani ni mrefu, umri nao umesogea sana,mwili na akili havimudu tena mapambano, busara zimuongoze aachie vijana chama,
katika waliobaki HECHE namuona anafaa zaidi kuliko hata Lissu.
 
Hivi kwanini mtu una support Chama fulani ?
  • Ideology ?
  • Watu waliopo ?
  • Fashion ?
  • Sababu huwapendi wengine ndio unaamua kwenda pengine ?
Nadhani Tanzania ideologically ni kama vyama vyote ni sawa kwahio watu wanafuata personalities au ulaji..., In short political infrastructure as is..., leaves a lot to be desired...

Huenda manufaa ya Taifa politically ni kwanza CCM kufa na kuzaliwa hata vyama 15 kutoka CCM..., na baada ya hapo kupata level playing field na kufuta ruzuku zote (atleast tutapata advantage moja ya kuokoa matumizi ya kodi zetu)
 
Hawa jamaa ni wahuni na walafi hawafai hata kidogo
 
Ndani ya chama lazima mkubali constructive criticism, kama Kuna pesa chafu au rushwa lazima mkubali mjikosoe. Ninachokiona kwa chadema hakina utofauti na kile wanachofanya ccm. Ukikosoa wewe unakuwa adui wao. Matokeo yake chama kinarudi nyuma hatua 100.
 
Sasa ni dhahili kuna Pesa chafu zinawatafuna CDM, Tundu Lissu ametoa hoja zenye mashiko. Badala ya kukaa kwenye kamati kuu na kujadili kwa kina na kisha kutoka na maazimio ya pamoja, yanaibuka MAGENGE YA VIJANA WAHUNI na kujibu kwa kejeli na mafumbo. Kwakweli Mbowe na vijana wake wanatukatisha tamaa kabisa.
 
Acha mambo ya ubaya ubwela,toka lini,mambo ya kutunga hayana tija.Je umewahi kukenua hayo unayosema ndani ya vikao rasmi vya chama?
Au unadhani Chadema ni kituo cha wasiojiweza,au jeshi la akiba?
 
Hii taarifa haikuhitajika kabisa. It is uncalled for and totally unwarranted. Hapa ndipo tunasema silence is gold.

Wafuasi na wengi wenye kuiunga mkono CHADEMA hawahitaji utetezi wowote wa uozo ndani ya chama. Sio wajinga. Hakuna dharura kwenye hilo. CHADEMA sio serikali kwamba maamuzi yake yana athari za dharura za moja kwa moja kwa wananchi. Mambo yakiharibika yatajulikana tu na uongo dhidi ya chama na viongozi wake utajulikana tu katika muda muafaka.

Viongozi watatue matatizo yao ndani ya chama bila kelele. Sisi tunaounga mkono chama tuone mwelekeo chanya wa chama tu. CHADEMA ina hazina kubwa sana ya watu makini na jasiri. Hatutegemei watu wawili watatu waonekane pekee ndio CHADEMA halafu waanzishe malumbano hadharani kutafuta kuungwa mkono. For what?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…