Pre GE2025 CHADEMA haina Uwezo wa kuweka Mawakala kwenye vituo vyote vya Uchaguzi kwahiyo kilio cha kuibiwa kura hakitaisha hata wasipoibiwa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu tunawezaje kuweka mawakala na wagombea leo kwa uchaguzi wa 2025? tupe mbinu
Hili hapa siyo jambo jipya, limejadiliwa oka zamani humu humu ndani ya Jukwaa hili hili, halafu leo linafanywa kuwa kama ni jambo geni?

Tulisema, toka mwanzo; huko 2015, na pengine kabla ya hapo kwamba kwa chama kama CHADEMA kilipofikia, ni dhambi kubwa kutoweza kuweka wagombea katika kila ngazi, tokea huko mitaani.
Tumekuwa tukibainisha kila wakati, kwamba hakuna siri; CCM inawategemea sana watu wake toka huko chini. Muundo huo wa CCM ndiyo sumu inayo maliza upinzani nchini. Tukashauri, kuiga siyo jambo mbaya. Igeni muundo huo, muwe na watu wenu huko huko, katika ngazi zote. Mtakosa vizi wasimamizi wa uhakika kama mnao watu wanao amini chama chenu tokea huko chini?

Sasa hapa tulipo, tunakumbushana tena yaliyokwisha zungumzwa na hayakutimizwa?

Mmekwisha waachia CCM mwanya wa kuendelea kuwateka waTanzania.

Inasikitisha na kuudhi kwa wakati mmoja.
 
Kasimu Majaliwa, Nape Nnauye, January Makamba, Riziwan Kikwete walipita bila kupingwa kwa vile Chadema haikuwa na wagombea? au unataka tufumue mambo ya aibu hapa? Waziri Mkuu wa Nchi gani ulisikia anateka Wagombea wengine?
Kama nakumbuka vizuri mpinzani wa Nape aliwekwa lock up siku ya kurudisha fomu!

Amandla...
 
Je, mgombea binafsi anaweza? Je, mkono wa Mungu hauwezi kukatwa? Na "wapigieni kura upande ule mwingine lakini mjue CCM ndiyo itaunda serikali"-mama Samia.
 
Wakala anasaidia nini kama Msimamizi wa Uchaguzi anajificha siku ya kurudisha halafu anaibuka kutangaza kuwa mgombea fulani amepita bila kupingwa?

Amandla...
 
Wakala anasaidia nini kama Msimamizi wa Uchaguzi anajificha siku ya kurudisha halafu anaibuka kutangaza kuwa mgombea fulani amepita bila kupingwa?

Amandla...
Mtoa mada amekosea sana. Kura hazipaswi kuibiwa hata kama baadhi ya vyama au wagombea hawana mawakala. Mimi naona hili ni jambo la aibu sana hata kulijadili. Ukisikia kuichafua nchi basi mfano mmoja ni kama huu wizi wa kura tunaoujadili. Hivi adhabu kwa mtu aliyepatikana na hatia ya wizi wa kura ni kifungo miaka mingapi?
 

Kwahiyo wasipoweka wakala mtawanapenauye eti! Pia niulize hakuna chama kingine cha kishauri ni Chadema tu? CCM je? ACT je? Kwani Chadema wasipoweka wakala wataibiwa kura na nani? Kwani kura lazima zilindwe Nan mwizi!
 
Nini kifanyike?
Sina hakika tena kama CHADEMA bado itakuwa na uwezo wa kuitikisa CCM hapa tulipo fikia sasa hivi kabla ya chaguzi; kwanza 2024, ambao kwa kweli ndio uandalizi wa ushindi wa 2025.
Sioni ni kwa njia zipi CHADEMA inaweza kujinasua kwenye kukabwa shingo ilikofanyiwa na CCM ya 'Chura Kiziwi'.
Mageuzi ya kukitikisa chama hicho kutoka katika hali hiyo siyo rahisi kuyafanikisha katika muda mfupi huu. ulio salia.

Je, tutazame huko huko ndani ya CCM? 'Chura Kiziwi' kajitahidi sana kuwabana wale waliokuwa na Magufuli. Kunawezekana kukaibuka wazalendo wa kweli wakakataa kunadishwa huku tunakofanywa na huyu 'chura?

Vyovyote na iwavyo, hata 'chura' akifanikiwa, na akaendelea na haya haya anayofanya sasa, tutegemee mtikisiko mkubwa ndani ya miaka hiyo mitano.
Hili halita epukika.
 
Kwahiyo wasipoweka wakala mtawanapenauye eti! Pia niulize hakuna chama kingine cha kishauri ni Chadema tu? CCM je? ACT je? Kwani Chadema wasipoweka wakala wataibiwa kura na nani? Kwani kura lazima zilindwe Nan mwizi!
LOOooh! unakuja hapa kufundishwa somo au vipi. Maswali unayo uliza hata hayaeleweki!
 
Katika hili tunapaswa kulaumu vyama au chama wezi wa kura, na sio kulaumu vyama au wagombea wanaoibiwa kura.
 
Wizi wa kura, au hujuma ya aina yoyote ktk zoezi la kupiga na kuhesabu kura, iwe ni kosa lenye adhabu kali ya kifungo.
 
Mkuu tunawezaje kuweka mawakala na wagombea leo kwa uchaguzi wa 2025? tupe mbinu
Wizi wa kura ni mchakato na unahusisha vitu vingi,inabidi kupitia indicators na variables zote kisha muone namna ya kuzuia hata hilo la uwepo wa wakala genuine kila kituo. Chadema fanyeni uchunguzi na tafiti kisha matokeo myafanyie kazi.
 
Mkuu ondoa shaka, nimekwishasema mara kadhaa humu kwamba ccm haitapata tena mwanya wa uchafu wa awali, hatutaki Mchengerwa mkwe wa chura kiziwi kusimamia uchaguzi (Hatutanii).

Kanda ya Nyasa tunao uhakika wa kuchukua majimbo 20 kati ya 31, hatutanii na tumefanya mambo tayari, ndio maana tulimuondoa Msigwa huyu alikuwa kikwazo (nitafafanua wakati mwingine), Chadema iko mpaka chini kabisa, mimi niko kwenye timu ya kuandaa mnyororo toka chini kwa miaka mitatu sasa, nafahamu ninachoandika, Tukiwabana kwenye wizi ccm haitoboi, ndio maana Hata Waziri mkuu anateka wagombea wa upinzani, anajua bila hivyo hashindi,

Tunajua kura walizopata 2020, hawana watu wanategemea polisi ambao nao wamechoka kabisa, tutatumia mataifa mbalimbali kuwadhibiti na Tumejipanga

Nasikitika kwamba Siwezi kuanika hapa kila kitu
 
Wizi wa kura ni mchakato na unahusisha vitu vingi,inabidi kupitia indicators na variables zote kisha muone namna ya kuzuia hata hilo la uwepo wa wakala genuine kila kituo. Chadema fanyeni uchunguzi na tafiti kisha matokeo myafanyie kazi.
Hakuna ambacho hatujafanya katika unayoleta sasa hivi tunapambana na wasimamizi wa uchaguzi tu na tutaweza
 
Tukiwabana kwenye wizi ccm haitoboi,
Kwa nini usiyaandike haya maneno kwa herufi kubwa!!

Kila mTanzania anajua hili. Yule 'Masabuni' Waziri wa Mapolisi anafanya yake, hakuna jibu. Haya ndiyo yanayotia wasiwasi kubwa. Maneppy naye anakuja kujaribu kupima kina...

Lakini ninalojua sasa na kuliamini, iwe CHADEMA au mwingineyo, CCM mwisho wao umewadia.

Nitanyamaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…