Pre GE2025 CHADEMA hali inazidi kuwa tete. John Mrema asema kama kuna ushahidi wa tuhuma za Rushwa uwasilishwe haraka kwaajili ya hatua za kinidhamu

Pre GE2025 CHADEMA hali inazidi kuwa tete. John Mrema asema kama kuna ushahidi wa tuhuma za Rushwa uwasilishwe haraka kwaajili ya hatua za kinidhamu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Mambo yanazidi kuwa ya moto, kama ndani kwa moto, nje wataweza kweli kuzima moto? Watatoboa kweli November 27?

===

1731592019907.png

CHADEMA kimejitokeza hadharani kukanusha vikali tuhuma zinazohusishwa nacho, hasa kuhusu madai ya rushwa na ufisadi yanayoelekezwa kwa baadhi ya viongozi wake na yanayodaiwa kujitokeza ndani ya chama hususan katika chaguzi za ndani.

Taarifa hii imetolewa siku ya Alhamisi Novemba 14, 2024 na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho John Mrema ambapo amesema;

Kupata taarifa za kimkoa kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ingia hapa:
LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

“Tuhuma za CHADEMA kuwa na fedha chafu au rushwa ndani ya Chama au katika chaguzi za Chama. Tuhuma hizi zimekuwepo maeneo kadhaa, baadhi zimekosa vielelezo vya ushahidi wa kisheria na maeneo mengine bado uchunguzi wa ndani unaendelea”, ameeleza Mrema katika taarifa hiyo.

Mrema akaendelea na kusisitiza kuwa:

“Chadema imekuwa mstari wa mbele kupambana na ufisadi, ubadhirifu na rushwa miaka yake yote. Kama Chama kikiletewa ushahidi au vielelezo vya tuhuma hizo kutoka kwa mtu yeyote tutafanyia kazi haraka iwezekanavyo kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na Mwongozo wa Chama dhidi ya Rushwa wa Mwaka 2012”.

Pia soma
- Lissu abanwa vikali na Mwana CHADEMA kuhusu tuhuma za rushwa ndani ya chama

- Kuelekea 2025 - LGE2024 - Wilbroad Slaa awavaa Tundu Lissu na Mbowe. Asema kuna rushwa CHADEMA na viongozi wake wako kimya tu!

Credit: Jambo TV
 
Mke wa Kigali ni VITI maalum Covid 19 sio rushwa.

Mke wa Salumu Mwalimu ni VITI maalum COVID-19 hii sio rushwa?

Mademu za Mbowe 10 ni VITI maalum pale Covid 19 hii sio rushwa?

Waanzie hapa tafadhali.
 
Mke wa Kigali ni VITI maalum Covid 19 sio rushwa.

Mke wa Salumu Mwalimu ni VITI maalum COVID-19 hii sio rushwa?

Mademu za Mbowe 10 ni VITI maalum pale Covid 19 hii sio rushwa?

Waanzie hapa tafadhali.
Bila aibu waliendaga mahakamani kuzuga
 
CCM Wana propaganda za kipumbavu mno! Rushwa si issue, issue ni kuenguliwa kwa wagombea wa CCM! Tuache upumbavu
 
Back
Top Bottom