Hamduni
Senior Member
- Apr 25, 2020
- 172
- 118
Tangu mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulipoanza, sijaona viongozi wa CHADEMA wakieleza mkakati wa kushiriki na kushinda uchaguzi huo. Badala yake, wamejikita kwenye malalamiko dhidi ya CCM na serikali.
Hakuna hata mchakato wa wazi uliotumika kuwapata wagombea ndani ya chama. Walikaa kusubiri wale waliokosa kuteuliwa ndani ya CCM, ndipo wakawachukua na kuwaomba wagombee kupitia CHADEMA.
Soma pia: CHADEMA: Baada ya Waziri wa TAMISEMI kusema Wagombea walioenguliwa wakate rufaa, tumepokea taarifa ofisi za Mitaa, Vitongoji na Vijiji zimefungwa
Cha kushangaza zaidi, hata katika ngazi ya makao makuu ya CHADEMA yaliyopo Mikocheni, hawajasimamisha mgombea. Badala yake, wamejikita kwenye kuilalamikia CCM, ambayo ilifanya michakato ya ndani na kuchagua wagombea kwa kura za maoni kwa wanachama wake nchi nzima.
CHADEMA wanahitaji kurudi mezani, kuangalia wapi wanakosea kama chama, badala ya kuendelea kulaumu serikali na CCM.