Uchaguzi 2020 CHADEMA hapa mmechemsha, badilisheni mikakati

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
6,905
Reaction score
4,054
Natoa ushauri kwa kuwa siipendi CCM na Mimi Sina chama ila napenda haki kwani haki huinua taifa.

CHADEMA kufanya uzinduzi sehemu tatu kwa siku tatu sehemu moja inachosha.

Watu waliokuepo leo Segerea si Jambo POA kwa mgombea uraisi.

Nadhani mlipaswa mfanye mobilisation mfanye uzinduzi ambao ni great once. First impression matters. Nilishawahi fanya interview naelewa

Nashauri wasije rudia hii kitu mikoa mingine kufanya kampeni sehemu ambazo zipo jirani kwa siku 2 au 3 haitakua poa.

Ni ushauri cause nyie ndio alternative ya CCM
 
Mahudhurio yalikuwa mazuri, labda kama lengo ni kupata nyomi na sio kufikisha sera. Mimi binafsi nilitaka cdm wafanye kampeni kwa kanda kwanza kwenye awamu ya kwanza, yaani Dar mkutano mmoja, kisha Arusha mkutano mmoja, Mwanza na Mbeya. Halafu waendelee wabunge kwenye maeneo yao. Kisha mgombea wa CHADEMA awe na mdahalo kwenye TV wangalau mara moja kila wiki kwa wiki 2. Kisha atoke awamu ya pili kwenda kanda ya magharibi, kanda ya kati na kanda ya kusini. Arudi tena awe na midahalo miwili kwenye TV. Halafu apite zile sehemu zenye washabiki wake wengi ambazo atakuwa hajapita.

Nilichogundua kwenye kampeni za kipindi hiki, ari ya watu kisiasa imeshuka sana kwa wananchi. Hii ndio sababu ccm inatumia zaidi wasanii kwani imejua bila hivyo vivutio, idadi ya wahudhuriaji inakuwa ndogo sana. Na ushukaji huu wa ari ya wananchi kwenye siasa, itasababisha uchaguzi huu kuwa na wapiga kura wachache sana. Rejea idadi ndogo sana ya wapiga Kura. Na yote haya yamesababishwa na rais aliye madarakani kutokutaka siasa kufanyika nchini, lakini aliyetaka chama chake pekee ndio kifanye siasa huku kikiwa hakina mvuto.
 
Ni kweli kabisa watu hawajawa na mwamko wa siasa kwa kipindi kirefu ndio maana mahuzulio yanadoda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…