Uchaguzi 2020 CHADEMA hapa mmechemsha, badilisheni mikakati

Ndio wanajifunza ikifika 2025 wanafanya vizuri zaidi kama watakuepo

Mwanzo wa ngoma ni lele.
 
Kupanga ni kuchagua,lazima tuwe na ndege na viwanja muhimu
Kapanga Magufuli,ndo maana Atcl haiwi audited,pesa zote zinazopangiwa matumizi na watanzania huwa audited na CAG
 
Mkuu ina maana hata mwenyekiti wako huwa humsikilizi? Magu yupo kwenye Vita kwa miaka mitano Sasa au wewe mwenzetu haupo nchini?
Kwahiyo Lisu kasema atatusiruhisha na nani?
 
Kwa Hilo limetokea kwa sababu kadhaa,miongoni ikiwa leo ilikuwa no siku ya umaa pale taifa hivyo tuligawana majukumu tuu,Ila mioyo yetu no yeye2020
 
Mkuu tunaendelea kuchanga huku ikibidi CHOPA ishambulie angani hawa watu TAYARI upepo
Chopa wataitungua CCM acha kabsa CCM ujue wana nia ya kuwahujumu chadema cyprian Musiba kila siku anapeleka njia mbalimbali za kumshambulia Tundu lisu tena, chadema mkimuona cyprian Musiba na Le mutuz huko mitaani mzomeeni kwa nguvu kubwa mpeni makavu live anataka kufanya walichomfanyia filipu njombe
 

Ukitaka kujua Magufuli kaharibu mwenendo wa siasa nchi hii, angalia kwa sasa mijadala sio sera tena, bali ni idadi ya watu kwenye mikutano. Juzi ccm wamefanya uzinduzi wa kampeni yao, lakini 80% ya waliohudhuria hawakujali sera, bali walikuwa wanajadili idadi ya watu na matukio ya uwanjani. Mfano tukio la Makonda kuzuiwa kukaa jukwaa kuu linafahamika kuliko hata alichoonge mwenyekiti wa ccm.

Kinachonitisha zaidi nenda kwenye vyombo vya habari kama redio na TV, hakuna mijadala ya uchaguzi kama ilivyokuwa hapo kabla ya Magufuli kuwa rais. Hakuna popote watu wanajadili mafanikio na mapungufu ya hii miaka mitano, na yapi matarajio siku zijazo. Ahadi zinatolewa lakini hazina ufafanuzi wowote,wala hakuna mjadala wowote wa maana kujadili ahadi za wagombea, bali kila mgombea anasema anachotaka kisha watu wanahamia kwenye idadi ya watu.

Haya mambo huwa yanaanza kiutani utani, ila tukishitukia tutajikuta tuna taifa la watu wasioweza kuhoji, bali viongozi tena wanaopita bila kupingwa wanakuja kutekeleza watakacho. Tutakapoanza kuwa ni viongozi wasiohojiwa, wala kuchaguliwa, tutarudi kule kule kwenye enzi za wahujumu uchumi. Na kwa mwenendo huu tutarajie idadi ndogo sana ya wapiga kura, kama unajaza watu kwenye mikutano kwa, ajili ya wasanii, siku ya kura hakuna wasanii, wapiga kura watatoka wapi?
 
Umeongea kitu sahihi,ari ya wananchi imeshuka sana.Nilikuwepo uwanja wa liwiti Tabata, mahudhurio ya watu hayakuwa mabaya sana ingawa pia hayakuwa makubwa sana.Pia vyama vya upinzani kutokupata coverage ya kutosha hasa kwenye TV station pia ni chanzo maana kuna watu hawapati taarifa za uwepo wa hiyo mikutano kwa wakati muafaka.
 
Mkuu mlihamasishana msiende kujiandikisha!
.
Hilo lilikuwa goli la kwanza kufungwa.

Hili la kuhamasishana ni bora ukae kimya, tume wana idadi ambayo hata tungehamasishana isingefika. Tunaposema tume hii sio huru, na awamu hii wamebobea kwenye kupika data hatukosei. Kwa taarifa yako hata kama kujiandikisha kupiga kura ingekuwa lazima kama kusajili line za simu kwa alama ya vidole, bado idadi isingekuwa 29m+. Nadhani unaelewa nini naongea.
 
Wapiga kura tutakuwa wengi Sana kwa kuwa tuna Jambo letu.kuwatondoa Tena kwa aibu wasioteda haki ,nakutudanganya no watetezi was wanyonge.
 
Vyombo vya habari vimezuiwa na CCM kuwaonyesha chadema
 
Mkuu kwani sera ni nini? Na Lissu kusema akiwa rais atarudisha Uhuru na haki ya watanzania kujiamulia Mambo yao wenyewe kinatofauti gani na hizo unazoita sera? Au kwako wewe sera ni kuwaahidi wateja wa TASAF kwamba utanunua ndege 5?
Wao wanataka tunakusanya kuliko awamu zote, tumejenga viwanda nchi nzima kuliko awamu zote, flaiova kira mahari, maji asirimia sabini vijiji vyote nchi nzima na asrimia tisini mijini. Sasa kirichobaki ni ndege tano ilikusudi tuzipite nchi zote Africa. Hizo ndo wanajua ni sera.

Habari za Uhuru, haki, maendeleo ya watu, bima za afya, mifumo ya elimu, mifumo bora ya uongozi na utaawala was sheria hizo kwa wengine ni adithi ambazo hawajawahi kuzoea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…