Mahudhurio yalikuwa mazuri, labda kama lengo ni kupata nyomi na sio kufikisha sera. Mimi binafsi nilitaka cdm wafanye kampeni kwa kanda kwanza kwenye awamu ya kwanza, yaani Dar mkutano mmoja, kisha Arusha mkutano mmoja, Mwanza na Mbeya. Halafu waendelee wabunge kwenye maeneo yao. Kisha mgombea wa Cdm awe na mdahalo kwenye TV wangalau mara moja kila wiki kwa wiki 2. Kisha atoke awamu ya pili kwenda kanda ya magharibi, kanda ya kati na kanda ya kusini. Arudi tena awe na midahalo miwili kwenye TV. Halafu apite zile sehemu zenye washabiki wake wengi ambazo atakuwa hajapita.
Nilichogundua kwenye kampeni za kipindi hiki, ari ya watu kisiasa imeshuka sana kwa wananchi. Hii ndio sababu ccm inatumia zaidi wasanii kwani imejua bila hivyo vivutio, idadi ya wahudhuriaji inakuwa ndogo sana. Na ushukaji huu wa ari ya wananchi kwenye siasa, itasababisha uchaguzi huu kuwa na wapiga kura wachache sana. Rejea idadi ndogo sana ya wapiga Kura. Na yote haya yamesababishwa na rais aliye madarakani kutokutaka siasa kufanyika nchini, lakini aliyetaka chama chake pekee ndio kifanye siasa huku kikiwa hakina mvuto.