Uchaguzi 2020 CHADEMA hawana mikakati thabiti ya kufanya kampeni

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Natumaini mko wazima. Nimeona nitumie haki yangu kikatiba kutoa maoni kuhusu kampeni za uchaguzi mkuu zinazoendelea.

Niseme kwamba iko wazi CCM wako kimkakati zaidi kwenye kampeni zao. Hawafanyi makosa kirahisi. Ila tatizo ninaloliona ni upande wa upinzani kwa CHADEMA. Kwa kweli mwenendo wao hauridhishi kabisa. Kampeni zao mwaka huu bora hata za mwaka 2005 alipogombea Mbowe.

Mgombea Tundu Lissu ni mgombea mwenye sifa nyingi nzuri kuendana na siasa za wakati huu. Ila timu ya kampeni ya CHADEMA imeonesha udhaifu wa hali ya juu. Ubaya ni kwamba wanajitahidi makosa yao kuwasingizia wengine. Mfano hai ishu ya chopa na TCAA.

Nahitimisha kwa kumsihi Comrade Humphrey Polepole awashauri jambo ndugu zetu wa CHADEMA ili kunogesha kampeni hizi. Mimi nadhani Polepole atakuwa hajafanya vibaya kuwasaidia hata mawazo ili angalau kutopoteza hata hizi kura chache wanazotarajia kupata.

CCM italaumiwa sana baada ya uchaguzi endapo CHADEMA hawataambulia chochote.

Pia nakemea vikali wananchi wasiojitokeza kwenye mikutano ya CHADEMA. Tafadhali wananchi wenzangu hasa wa Bagamoyo tusiwasuse kabisa.

Muhimu ni tarehe 28 kuwanyima kura wapinzani.
 
Kamshauri jiwe aache kilugha kwenye kampeni analigawa taifa kwa ukabila.
 
Reactions: BAK
Hueleweki kama mwenyekiti wako wa chama hata kiswahili ni shida, ccm ni kama kundi la viumbe flani wanaofanana kwa ujinga na ujanja, huwezi kutofautisha profesa na la saba wote wanavyotetea upuuzi, utadhani kuna mda wanashauri kuongea pumba
 
Hueleweki kama mwenyekiti wako wa chama hata kiswahili ni shida ,ccm ni kama kundi la viumbe flani wanaofanana kwa ujinga na ujanja ,huwezi kutofautisha profesa na la saba wote wanavyotetea upuuzi
Yaani kwa CCM yetu ni kama vile hakuna MAISHA nje ya madaraka. Mazoea mabaya kweli hayo. Yamevuruga hadi chaguzi zetu. Sasa wanataka vyote kabisa. Urais, Bunge na Halmashauri zote kabisa. Vijiji na mitaa walishachukua vyote.
 
Reactions: BAK
Kufanya Kampeni kwa kutumia kilugha ni kukiuka sheria za uchaguzi hivyo JIWE hana budi kuadhibiwa.
 
Reactions: BAK
Yaani kwa CCM yetu ni kama vile hakuna MAISHA nje ya madaraka. Mazoea mabaya kweli hayo. Yamevuruga hadi chaguzi zetu. Sasa wanataka vyote kabisa. Urais, Bunge na Halmashauri zote kabisa. Vijiji na mitaa walishachukua vyote.
Hawawezi tena majimbo wabunge na madiwani wa upinzani wameenguliwa karibu wote wameanza kurudishwa sasa ,wabunge wa CCM hawakosei fomu Tz nzima upinzani tu ndo wanakosea.Yaani wana akili za kuvukia barabara
 
Reactions: BAK
Muheshimiwa Polepole kachaguliwa na wananchi? Majinga ya CCM hamuwezi kutofautisha Ndugu na muheshimiwa arrghhh
 
Asante kwa taarifa
Your browser is not able to display this video.
 
Atakayeelewa anibeep.
Mimi nimemwelewa ila wewe na wenzio, wajuvi wa kujadili watu na kushabikia matukio, hamwezi kumwelewa.

Jaribu kuieleza, kwa ufasaha, Sera ya Haki, Uhuru na Maendeleo ya watu hapa! Hata mgombea wenu Lissu, wa Urais anataja tu falsa za Baba wa Taifa bila kuzifafanua, kwa sababu hajui misingi yake. Nazo ni:
Uhuru na Kazi
Uhuru na Maendeleo
Uhuru na Umoja

Anaropoka akiamini wanaomsikiliza ni wazee wa baraza za mahakama ambao huwababaisha kwa lugha za kisheria. Akumbuke tu kuwa wapiga kura ni pamoja na wasomi waliobobea kwenye sayansi ya jamii na taaluma zingine.
 


Wewe ni mwanachadema? Kama ccm wapo kimkakati zaidi unatakiwa kufurahi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…