MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Natumaini mko wazima. Nimeona nitumie haki yangu kikatiba kutoa maoni kuhusu kampeni za uchaguzi mkuu zinazoendelea.
Niseme kwamba iko wazi CCM wako kimkakati zaidi kwenye kampeni zao. Hawafanyi makosa kirahisi. Ila tatizo ninaloliona ni upande wa upinzani kwa CHADEMA. Kwa kweli mwenendo wao hauridhishi kabisa. Kampeni zao mwaka huu bora hata za mwaka 2005 alipogombea Mbowe.
Mgombea Tundu Lissu ni mgombea mwenye sifa nyingi nzuri kuendana na siasa za wakati huu. Ila timu ya kampeni ya CHADEMA imeonesha udhaifu wa hali ya juu. Ubaya ni kwamba wanajitahidi makosa yao kuwasingizia wengine. Mfano hai ishu ya chopa na TCAA.
Nahitimisha kwa kumsihi Comrade Humphrey Polepole awashauri jambo ndugu zetu wa CHADEMA ili kunogesha kampeni hizi. Mimi nadhani Polepole atakuwa hajafanya vibaya kuwasaidia hata mawazo ili angalau kutopoteza hata hizi kura chache wanazotarajia kupata.
CCM italaumiwa sana baada ya uchaguzi endapo CHADEMA hawataambulia chochote.
Pia nakemea vikali wananchi wasiojitokeza kwenye mikutano ya CHADEMA. Tafadhali wananchi wenzangu hasa wa Bagamoyo tusiwasuse kabisa.
Muhimu ni tarehe 28 kuwanyima kura wapinzani.