CHADEMA hii ni fursa nyingine ya Chama kuimarika zaidi

CHADEMA hii ni fursa nyingine ya Chama kuimarika zaidi

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Waingereza walisema what does not kill you, leaves you stronger. Tukio baya ambalo halikusababisia kifo, hukufanya kuwa imara kuliko hapo mwanzo.

CHADEMA kimepitia misukosuko mingi lakini chama hiki kimebaki kuwa imara zaidi kuliko siku za nyuma. Kuna kipindi miaka kama 8 hivi iliyopita chama hiki kilipita katika giza la uvuli wa mauti na wengi walifikiri kuwa huo ndio mwisho wa CHADEMA, lakini haikuwa hivyo.

CHADEMA leo ni chama imara kuliko wakati ule. Na hata wakati huu ambapo wapo watu wanaotarajia kusambaratika kwa chama hiki, habari mbaya kwa watu hawa wasiopenda kuona upinzani imara nchini ni kwamba, mbinu wanazofanya kuidhoofisha CHADEMA ndio makosa yao makubwa kisiasa, kwani CHADEMA ndio kwanza inaimarika.

Soma Pia: Mpasuko wa CHADEMA tatizo ni Asali, Ukabila na Uenyekiti Taifa

Ni wakati mzuri kwa chama kujipepeta na kutupa makapi mbali na kubaki na mchele. Wana CHADEMA hiki ni kipindi kingine cha kukua na kukomaa zaidi. Wanaokitakia chama kifo watakufa wao na kuiacha CHADEMA hai na yenye nguvu zaidi kuliko jana.
 
Wana Chadema wote wahamie CCM na wagombee uongozi kupitia Ccm wakishapata uongozi waweke mazingira mazuri ya kisiasa kisha wooooote wanarudi zao Chadema. au vipi
 
Back
Top Bottom