TL kawachanganya hasa. Mmejikuta hamna legal Avenue ya kumstop asiwavue nguo. Hamna strategy ya kiushindani kupambana naye. Zaidi ya kupanga uovu wa gizani kama mazowea yetu.
Si polisi, Usalama wa Taifa, wachawi wenu, death squad zenu, green guard. na kila nguvu ya giza mnayotumia vyote havifui safu.
Sembuse na vi propaganda uchwara hivi mnavyohangaika navyo huku kwenye social media? Hamtaweza. Wala msihangaike kuharibu amani ya nchi bure. Subirini mjaribu bahati yenu kwenye kujumlisha kura za urais ambapo siku zote huwa mnapitia.
Huku kwingine msipiteze muda. Mtaangamiza hili taifa na ninyi wote hamtafaidi lolote.
Hivi mbona hamjadili matatizo makubwa yanayownyemelea ndani ya CCM? Myaivuka hiyo mitego mliyowekewa? Mlifocus kwa wapinzani mkasahau mlivyo weak ndani. Mmeingiziwa wapiga kazi ndani na hamtoki salama. Huenda game mkaimaliza wenyewe huko bila hata TL kutumia nguvu nyingi kwenye kampeni.
Endeleeni mtagundua.