Tman Clever
Member
- Dec 20, 2012
- 39
- 29
Kwenye Uchaguzi huu wa CHADEMA Kuna mambo kadhaa ya kuzingatia kuhusu Hawa wagombea wa uenyekiti.
Freeman Mbowe
STRENGTH
1. Hekima zake,mikakati,kujitoa kwake hata kiuchumi bado zinahitajika kwa CHADEMA na siasa za nchi hii
2. Uhakika wa kuto kununulika kwake kunafanya awe muhimu kuendelea kuwa Mwenyekiti, maana hatuna uhakika wa 100% na yeyote ajae kama hatonunulika na kukiua Chama.
WEAKNESSES
1. Mikakati yake imepitwa na wakati, haina uwezo wa kukipa Chama jambo jipya.
2. Alisha fanya yooote kwenye siasa,hasa mazuri, kama vile kuwavutia Wana siasa Nguli na wasomi wabobevu kwenda upinzani na Kisha kuwapoteza Tena. inahitajika mtu mpya kuendeleza na kuibua mapya
Tundu Lissu
STRENGTH
1. Mwana harakati mbobevu, Mwanasheria Nguli, anaogopeka na watawala,
2. Amesha jitanabaisha ni mtu asie na makandokando mbele ya umma, ndicho kinacho mpa uhalali zaidi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha upinzani, na ndicho kilicho ipaisha CHADEMA kuwa tumaini la wanyonge na wasakatonge.
3. Akifanikiwa kuwa Mwenyekiti, atazoa maelfu ya wanachama wapya na wafuasi hasa wanaoamini katika kupinga rushwa na ufisadi, CHADEMA itarudi kwenye iumara wake kwa kasi sana
WEAKNESSES
1. Ni mwana harakati zaidi kuliko kuwa kiongozi, kwa sayansi ya kawaida hato weza kukilea Chama chenye watu tofauti tofauti wenye fikra zinazotofautiana.
2. Mashaka inakuja kwa namna anavyo saidiwa zaidi na wasio wapiga kula halali wa CHADEMA, hajajibu ni Nani yupo nyuma yake,
3. Hajajua nini hasa cha kuzungumza na nini cha kuto kuzungumza mbele ya Kamera,
Ndio anatakiwa kuonesha amenyooka maana hivyo ndivyo alivyo na ndio iumara wake, lakini ndio udhaifu unao fanya asiwe kiongozi anaestahili kuiongoza Taasisi nyeti.
N.B: Kama ni kwenye dini, Basi Tundu Lissu ni Muinjilisti, na Freeman Mbowe ni Mchungaji
Mmoja anaweza kuwafanya watu wengi waokoke lakini hawezi kamwe kuwalea kwa pamoja, na Mwingine Hana uwezo wa kuwafanya wadhambi wengi waokoke, lakini akipewa kuwalea, basi atawalea wote kwa ufasaha mkubwa Sana.
Wapiga kula halali wa CHADEMA tunaamini mtafanya lililo bora na Kwa utulivu mkubwa.