nokwenumuya
JF-Expert Member
- Jun 29, 2019
- 820
- 2,901
Nimelike.Hakuna hakimu mwenye 'ethics' atakayemfunga mtu kwa ile kesi ambayo wauaji wanajulikana na hawakamatwi.
Muhimili wa mahakama ingawa unapata misukosuko mingi kutoka muhimili mwingine lakini sikuzote wamejitahidi kutoa hukumu za haki....kama sio mahakama ya chini mahakama ya juu yake.
Bado nina imani na mahakama zetu against all odds.
We unaijua hiyo hukumu?Hukumu imesha pitishwa tayari na ndiyo sababu ya CHADEMA kutoalikwa Ikulu.
Wewe mkata kachumbaru subiri uolewe Tu haya mambo ya siasa huyajuiHata wakifungwa hakuna mtanzania atakaye jitokeza kuwatete waharifu. Si mlijifanya kumtetea Kabendera, mmeishia wapi??? Yaani kutoka kupinga uharifu mpaka kuwa waunga mkono uharifu na ufisadi.
Hata wakifungwa hakuna mtanzania atakaye jitokeza kuwatete waharifu. Si mlijifanya kumtetea Kabendera, mmeishia wapi??? Yaani kutoka kupinga uharifu mpaka kuwa waunga mkono uharifu na ufisadi.
Mkuu ,lazima wafungwe,lakini kifungo kitakuwa kwenda jela au kulipa faini,watalipa faini ili kuogopa kwenda jela,wakikata rufaa haitasikilizwa hadi uchaguzi upite kwa hiyo hiyo hukumu itakuwa imewaondoa kwenye uchaguzi,maana watafungwa zaidi ya miezi 6.Hakuna hakimu mwenye 'ethics' atakayemfunga mtu kwa ile kesi ambayo wauaji wanajulikana na hawakamatwi.
Muhimili wa mahakama ingawa unapata misukosuko mingi kutoka muhimili mwingine lakini sikuzote wamejitahidi kutoa hukumu za haki....kama sio mahakama ya chini mahakama ya juu yake.
Bado nina imani na mahakama zetu against all odds.
THANKS SO MUCH SIR. BE BLESSEDLini umeteuliwa kuwasemea WATANZANIA? Kwa uelewa wako unafikiri kupinga jambo ni hadi iwe physical demonstration kujazana Kisutu! Tatizo lenu waimba mapambio mnafikiri Nchi ni mali ya Chama Cha Mapinduzi. Ile kesi ni more political, aliyesababisha disorder ni Mkurugenzi aliyepaswa kuhakikisha viapo vinafanyika kwa mujibu wa utaratibu, siyo kujificha ficha hadi atafutwe kwa watu kutembea kwenda ofisini kwake! Halafu watokee polisi waue yule binti, kesi irudi kwa viongozi wa chama cha CHADEMA!
Tuwe na hofu ya Mungu katika kutenda na kunena kwa mamlaka tuliyo nayo. Upinzani ni watu, 2015 waliopata kura, means kuna wafuasi nyuma yao. Leo mnapounga mkono DHURUMA na UONEVU kukomoa mkidhani Upinzani ni Mbowe & Co mnafanya kosa kubwa. Kuna chuki mnaipanda, mbegu inamea na Taifa litakuja kuvuna ZAO baya mno.
Ipo mifano ya wazi ya hizi kesi za kisiasa za KUTENGENEZWA ili tu mkosoaji wako asote jela, all dictators wanafanya hivi but in the end yanawarudia. Omar Al-Bashir na Ugandan former IGP leo wako wapi?
"Don't entrust a stupid man with power".
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ,lazima wafungwe,lakini kifungo kitakuwa kwenda jela au kulipa faini,watalipa faini ili kuogopa kwenda jela,wakikata rufaa haitasikilizwa hadi uchaguzi upite kwa hiyo hiyo hukumu itakuwa imewaondoa kwenye uchaguzi,maana watafungwa zaidi ya miezi 6.
Naweza kukubaliana na weweHukumu imesha pitishwa tayari na ndiyo sababu ya CHADEMA kutoalikwa Ikulu.
Mambosasa aliyeamuru Mauaji ya Akwilina na kukiri hadharani hajaguswa hadi leo !Hawa watu uelewa wao ni mdogo.Wanatisha mahakama isifanye kazi yao?
Kwamba wahalifu hao kama watatiwa hatiani amani ya nchi itatoweka?
What a nonsense?
---
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani kimewataka wanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani Tanzania kuanzia leo Jumamosi Machi 7, 2020 kuvaa nguo nyeupe au kufunga kitambaa cheupe kama ishara ya kutaka haki itendeke katika hukumu ya viongozi wa chama hicho Machi 10, 2020.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katibu wa kanda hiyo, Hemed Ali ametoa wito kwa wanachama wote kufanya hivyo kwa kuwa haki ni ya kila mtu.
Viongozi wanane wa Chadema pamoja na katibu mkuu wa zamani wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji wanakabiliwa na mashtaka 13 yakiwemo ya kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria na kusababisha woga na hofu kwa wakazi wa Kinondoni na kifo cha Akwelina Akwilini.
Jana viongozi wakuu na wabunge wa Chadema walifunga kazi baada ya kuwasilisha hoja zao za majumuisho katika kesi ya jinai inayowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wameiachia mahakama kufanya kazi yake.
Viongozi hao ni mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; katibu mkuu wa chama hicho, John Mnyika.
Wengine ni naibu katibu mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu; mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; Esther Matiko ambaye ni mweka hazina wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) na mbunge wa Tarime Mjini; Halima Mdee (mbunge wa Kawe); Ester Bulaya (Bunda); John Heche (Tarime Vijijini).
"Mavazi hayo meupe yatakuwa yakiashiria kupinga uonevu, watu tujitokeze kwa wingi siku ya hukumu pale mahakamani. Watakaoshindwa kukusanyika katika ofisi za Chadema basi wafanye midahalo ya haki siku hiyo.”
"Kuna wanawake zaidi ya 5,000 wanatoka mikoani wanakuja Dar es Salaam kwa ajili ya siku ya wanawake kesho, tumeongea na Baraza la wanawake Chadema wanawake hao wabaki hadi Machi 10 ili tuungane nao mahakamani," amesema Hemed.
Amesema siku hiyo ni siku ya kuonyesha amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania ili kupigania amani ya nchi aliyodai kuwa inapatikana ikiwa kuna haki.
"Hatupendi amani ya nchi hii iharibike lakini vilevile hatupo tayari kuona viongozi wa chama chetu wanaonewa, kesi yao hii ni kesi ya kisiasa," amesema.
Amedai kuwa hukumu yoyote ya kuwatia hatiani viongozi hao itazima amani ya nchini.
Chanzo: Mwananchi